Mkuu wa Wilaya ya Mufindi akipokea Risala ya Shirika la PDF
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William, akiwahutubia wananchi wa wakati wa uzinduzi wa mradi kata ya MbalamaziwaNA OFISA HABARI MUFINDI
Serikali
Wilayani Mufindi, imesema itaanza kuchukua hatua kali za kisheria zilizopo kwa
wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, wasiozingatia sheria
za afya ya mazingira, hususani suala la kuwa na vyoo, ambapo takwimu
zinaonesha kati ya kaya 59,152 za Halmashauri hiyo, zaidi ya kaya 7,00
hazina vyoo huku kaya zaidi ya 3,000 bado zinatumia vyoo vya asili.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh
Jamhuri William, katika kata ya Mbalamaziwa alipokuwa akizindua mradi wa Maji,
Afya, Lishe, usafi wa Mazingira sanjari na usafi wa Mtoto chini ya miaka 05 ukitekelezwa kwa pamoja
kati ya Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na shirika la (peoples Development
Forum) PDF chini ya ufadhili wa UNICEF.
Mh.
Jamhuri amesema ni aibu kwa muda wa miaka 55 ya uhuru bado kuna Watanzania wanajisaidia porini
au kwenye vyoo visivyo na sifa na kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira pamoja
na magonjwa ya mlipuko na kufafanua kuwa suala la kuwa na nyumba bora
linalozingatiwa na wakazi wa Halmashauri hiyo, ni lazima liende sambamba na
ujenzi wa choo chenye ubora huku akiahidi kuchukua hatua za kinidhamu kwa
watendaji wa Vijiji watakao zembea kusimamia suala hilo.
Katika
hatua nyingine Mh. Jamhuri William, amewataka wakazi wa Halmashauri hiyo,
kutumia vema uwepo wa aina mbalimbali za vyakula Wilayani humo, kuondokana na suala la lishe
duni licha ya Mkoa wa Iringa kuwa miongoni mwa mikoa 05 ya nyanda za juu
inayoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula, huku akitilia mkazo kuachana na
tabia ya kula unga wa Sembe badala ya dona yenye viinilishe hitajika.
BDF
Kwa kushirikiana na Halamashauri ya Wilaya ya Mufindi chini ya ufadhli wa
UNICEF, itatekeleza miradi hiyo katika kata nne za Mbalamaziwa, Ikweha, Sadani
na Mtambula, ambapo itachimba visima, kukarabati miradi ya Maji, Ujenzi wa vyoo
kwenye tasisi za umma pamoja na Usafi na lishe bora kwa Mtoto chini ya miaka 05
0 comments:
Post a Comment