Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa
albamu ya tatu ya TARATIBU NITAFIKA iliyoimbwa na Elineema Babu
Katika
uzinduzi huo, Mhe.Mtaturu ameendesha zoezi la uuzaji wa albamu hiyo iitwayo
TARATIBU NITAFIKA na kusaidia upatikanaji wa zaidi ya shilingi Milioni Tatu
ikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi ambapo ofisi yake imechangia jumla ya
shilingi milioni moja (1,000,000), huku Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani humo
kikiwa kimeunga mkono uzinduzi wa albamu hiyo kwa kuchangia shilingi laki tano
(500,000)
Mhe.Mtaturu
amewahimiza waimbaji wa nyimbo za injili wilayani humo kutumia vyema fursa
waliyonayo kwa kuimba nyimbo zenye kuhamasisha amani na upendo nchini, akitolea
mfano kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza iliyoimba wimbo uitwao AMANI kwa
ajili ya kuhamasisha amani nchini.
Alisema
kuwa tunu ya nchi ya Tanzania ni amani na upendo hivyo wachungaji pamoja na
waimbaji wa nyimbo za injili wanapaswa kutilia mkazo uhubiri wao kuhamaisha
Upendo, Amani na Mshikamano baina ya wananchi wote pasina kubagua itikadi za
kisiasa, dini ama kabila.
Mhe
Mtaturu alisema kuwa wanasiasa ambao wamepewa dhamana na wananchi wana jukumu
moja la kuwatumikia kwa kuwaletea maendeleo sio kuhubiri siasa na uchochezi
jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo yao katika kukuza uchumi wa mtu mmoja
mmoja na Taifa kwa ujumla.
Mwimbaji
Elineema Babu ameachia albabu ya tatu iitwayo "Taratibu Nitafika"
yenye nyimbo nane ambapo amewasihi wadau wengine kumsaidia kwa kununua albamu
hiyo (Audio) ili aweze kupata shilingi Milioni Sita zinazohitaji ili aweze
kurekodi video ya albamu hiyo. Taratibu Nitafika ni albamu ya tatu baada ya
kutanguliwa na albamu mbili ambazo ni Nitumie pamoja na Fanya Kazi ya Bwana.
Mwimbaji Elieneema Babu
akitumbuiza kwenye uzinduzi huo Agosti 20, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mhe. Miraji
Mtaturu akionyesha CD alizozindua wakati wa uzinduzi huo ambapo alikuwa mgeni
rasmi
DC Ikungi akizindua albamu hiyo
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe Miraji Mtaturu
(kushoto), akimkabidhi CD Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg
Philiph Elieza kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji Elineema Babu
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu
(kushoto), akimkabidhi CD Baba Askofu wa Jimbo la Singida Dkt.Paul Samweli
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe Miraji Mtaturu
(kushoto), akimkabidhi CD Mwenyekiti wa mtandao wa Wazo Huru Blog Ndg Mathias
Canal kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji Elineema Babu
BMG Habari
0 comments:
Post a Comment