METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, October 20, 2016

Kukauka kwa mto Ruaha kwamshangaza January Makamba








Na Daniel Kilonge, Iringa

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Muungano na mazingira Mhe January Makamba ametembelea hifadhi ya Ruaha National Park kwa lengo la kujionea baadhi ya rasilimali za eneo hilo zilivyo hatarini kutoweka .

Miongoni mwa rasilimali hizo ambazo ni pamoja na mto Ruaha ulivyo hatarini kupotea kabisa kutokana na kukauka kwa maji jambo ambalo halitoi ishara njema kwa hifadhi hiyo.

Akizungumza mbele ya Waziri huyo mwenye dhamana ya kusimamia mazingira Muhifadhi wa hifadhi hiyo amesema kuwa hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1992 mto huo kukauka kwa miezi sita mfululizo huku akitaja chanzo kuwa ni uchepushwaji holela wa maji wilayani Mbarali.

Katika Ziara yake iliyo ongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela, wamezindua zoezi la upandaji miti ambapo kwa pamoja wamepanda miti katika shule ya msingi Mlandege.

Mhe Makamba pia amesema Serikali ina mpango wa kuanzisha mkakati wa upandaji miti mashuleni ambapo kila mwanafunzi atatakiwa kupanda mti aingiapo shuleni na kulazimika kuutunza mti huo mpaka atakapo maliza shule.

Picha zote na Daniel Kilonge.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com