Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umesema matamshi ya kilofa na kipumbavu yaliotamkwa na Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema) Tundu Lisu ni ya kusaka umaarufu wa kisiasa hatimae awanie urais akiwawacha solemba Edward Lowassa na mshirika wake Fredrick Sumaye .
Aidha Umoja huo umesema povu linalowatoka viongozi wa upinzani akiwemo Lisu, ni kielelezo cha kutapatapa na kufilisika kisiasa kufuatia utendaji unaokubalika wa serikali ya Rais John Magufuli huku wakionekana kuvunjika matumaini na kukata tamaa.
Hayo yametamkwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati alipozumguza na viongozi, wanavyuo, makundi ya vijana, wanachama wa CCM na jumuiya zake katika ukumbi wa CCM Kizota mjini kigoma mkoani hapa.
Shaka alisema maneno ya Lisu hayawezi kuitingisha serikali ya CCM na kwamba serikali inayoinanga iwapo itamtaka akamatwe kwa kuvunja sheria za nchi, vyombo vya dola havitasita kumuweka kizuizini.
Alisema kuna kila ishara ya mwanasiasa huyo wa upinzani inayoonyesha akiyatamani maisha ya gerezani baada ya kuchoshwa na yale ya uraiani ambapo sasa ameamua kutamka upuuzi, kujeli kinyume na ustaarabu.
"Tumemtafakari na kubaini ana nia ya kuwania urais mwaka 2020, anachotaka ni kuwaacha kwenye mataa jamaa zake kina Lowasa na sumaye, ila ajue akizidi kueneza matamshi ya kipuuzi anaweza kukamatwa na kutupwa mahali"Alieleza shaka
Alisema hakutawakuwa hakuna maana ikiwa mtu mmoja anainanga Serikali na kuipaka matope, kumkejeli Rais aliyewekwa kisheria na kikatiba na wananchi akaendelea kutazamwa macho.
"Lisu si kama papai ambalo kama likiwekwa ndani litaooza na kuharibika, anaweza kukaa huko kwa usalama wake na wa nchi, tumeruhusiwa kisheria kufanya siasa za vyama vingi kwa ustaarabu na uungwana na si kufanyiana kejeli na dhihaka "Alieleza
Alisema hata wakati wa utawala wa Baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere walikuwepo baadhi ya wanasiasa waliotaka kuidharau serikali, walikamatwa kwa usalama wao na kuhifadhiwa mahali kwa muda fulani kwa maslahi ya nchi.
"Lisu ni nani mbele ya mamlaka za kisheria na kikatiba, tunadhani anataka nyingi nasaba hivyo ajiandae siku yoyote anaweza kukutwa na msiba, msiba wa kujitakia hauna pole, dola yoyote haifanani na kitambaa cha deki" Alisisitiza.
Uvccm ina ushahidi wa kutosha toka kwa watu wa karibu na Lisu wamemwambia kwamba ndiye anayetosha kuwania urais ndani ya chadema mwaka 2020 hivyo ametakiwa atafute "kick' ya kisiasa ili kumvuruga Sumaye na Lowassa .
Hata hivyo shaka alisema si kosa kwa Lisu kuwania urais ila anachotakiwa ni kujipima kibusara, kiuwezo na kiupepo kama ni mtu anayestahili na sahihi ambaye anayetosha kuomba nafasi hiyo au la.
Vile vile uvccm umewataka watanzania kumpuuza mwanasiasa huyo wa chadema kwa kadri atakavyotamka kwasababu mtu yoyote mwenye ufahamu na uelewa hawezi kudhihaki mamlaka ya Rais na nafasi alionayo.
"Ujasiri wa kuidhihaki mamlaka ya Rais ni sawa na mtu juha au punguani anayejaribu kutupa jiwe katikati ya mzinga wa nyuki au mpumbavu kumchezea simba sharubu "Alieleza shaka.
Kaimu huyo katibu mkuu Shaka aliwashukuru wazee wa mkoa wa kigoma kwa kumtawaza na kuwa mwana kigoma huku akiwahidi hatawangusha ila malipo anayoyaanda kuonyesha shukran na furaha yake ni kuongoza harakati za kisiasa zitakazomuondoa Zito Kabwe kwenye nafasi ya ubunge wa kigoma mjini mwaka 2020 .
0 comments:
Post a Comment