METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, July 16, 2017

UMOJA WA VIJANA WA CCM VYUO NA VYUO VIKUU MKOA WA MWANZA WAKAKABIDHIWA VYETI NA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA

Mgeni Rasmi Katika Mahafali ya wahitumu wa Vyuo vikuu Mkoa wa Mwanza Ndugu Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Rodrick Mpogolo , Akiongozana na Daniel Zenda K.katibu Idara Vyuo na Vyuo Vikuu , Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndgugu Anthony Dialo, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndg Raymond Mwalimu, Waheshimiwa Wabunge wa Ilemela na Nyamagana pamoja na viongozi wa secretariat ya Mkoa, Katibu wa CCM Nyamagana na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi, Makundi ya Kijamii, Machinga, wapiga debe, Mama Ntilie na wajasiliamali. Mahafali yaliyofanyika Ukumbi Rock City Mall.

Ndugu Mgeni Rasmi  amewasihi sana wahitimu kuwa Wabunifu wa miradi za kuweza kujitegemea haswa katika Kilimo na Ufugaji, Mgeni Rasmi aliwakumbusha wahitimu kuenenda sawa na Imani ya Ccm kama ilivyoainishwa katika katiba ya CCM Ibara ya nne (4) na   aliwataka wahitimu Wajiajiri(Blue colour Job) na kutumia Maarifa waliyonayo katika Jamii na kuondokana na dhana ya kuajiriwa.

Aliendelea kusisitiza Umuhimu wa Database yani taarifa za wahitimu wote zinaumuhimu sana kwa kutumikia chama cha Mapinduzi na Taifa kwa Ujumla.

Mahafali ya kwanza kubwa Mkoani wanafunzi/Makada walio hitimu 256 na washiriki walio hudhuria 612 wanachama.

Mahafali hiyo ilifana kwa kuanza Shughuli ya kijamii kutembelea kituo cha Watoto waliofanyiwa Ukatili(Foundation Karibu Tanzania) kaimu katibu Idara Vyuo na Vyuo Vikuu ndg Daniel Moses Zenda  aliongoza Shughuli hiyo na kujionea namna Ukatili waliofanyiwa watoto hao. Pamoja na kushiriki na kutoka Mchango Ulioandaliwa na Wanafunzi wa Vyuo Vikuu.

Imetolewa na
Idara Vyuo na Vyuo Vikuu.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com