Kupitia tangazo lake kwa umma, TCAA
imesema kuwa kwa taasisi au mtu binafsi kufanya majaribio au kurusha drones, ni
lazima apate idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mamlaka hiyo.
“Ifahamike kuwa kuanzia sasa, taasisi au
mtu binafsi anayetaka kununua, kufanya majaribio au kurusha angani vifaa hivyo
visivyotumia rubani anapaswa kupata idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama
pamoja na kibali kutoka TCAA,” imeeleza taarifa ya Mamlaka hiyo.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi
Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imefafanua kuwa uendeshaji wa shughuli zote za anga
nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.
Tangazo hilo linakuja wakati ambapo
kumekuwa na urushwaji wa drones unaofanywa na watayarishaji wa video za muziki
kwa lengo la kuchukua picha za juu, pamoja na taasisi mbalimbali zinazochukua
matukio husika hasa yanapofanyika katika maeneo ya wazi.
0 comments:
Post a Comment