Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene |
WAKUU wa Wilaya (DC) na Wakurugenzi
Watendaji (DED) wameonywa kuacha kutunishiana misuli na kuendeleza migongano
badala yake washirikiane kwani wanategemeana katika kutekeleza majukumu yao.
Onyo hilo lilitolewa na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene mjini Dodoma jana wakati
akifungua semina elekezi kwa ma-DC na ma-DED wa mikoa sita kutoka Kanda ya
Ziwa.
Akizungumza kabla ya kuanza mafunzo kwa
viongozi hao kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Simiyu, Manyara na Geita,
Simbachawene (pichani) aliwataka wachukuliane hali, hisia, tabia na wavumiliane
na kushirikiana badala ya kuonesheana ubabe na kila mmoja kujiona ana madaraka.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi),
Selemani Jafo aliwataka viongozi hao kutumia vizuri dozi watakayopata hapo
iwasaidie kwenda kutimiza majukumu yao vizuri na kuleta mabadiliko katika
maeneo hayo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mussa Iyombe aliwataka ma- DC na ma-Ded hao kujifunza kwa bidii katika semina hiyo kujua vizuri majukumu yao na mipaka ya kazi yao badala ya kukaa siku tano na kurudi watupu.
0 comments:
Post a Comment