Serikali
imesema kuwa inatarajia kuanza kutoa Chanjo ya Homa ya Ini kwa wananchi
wote bila kujali kigezo cha umri wala uwezo wa kifedha kwa wale wote
wenye dalili za ugonjwa au wenye ugonjwa wa Ini.
Hayo
yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza
kuhusu maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya ini duniani.
“Katika
kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani tumedhamiria
kuhakikisha chanjo ya ugonjwa huu inapatikana kwa watu wote nchini ambao
wana hatari ya kupata maambukizi ya homa ya ini au tayari wamepata
ugonjwa huo, watapata chanjo kwa bei nafuu kwa mswaka wa bajeti
2018/2019” alisema Ummy.
Alisema
kuwa ili kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini mpango wa
damu salama unatakiwa kuhakikisha wanapima damu zote za wachangiaji
kabla ya kuwawekea wagonjwa wanaohitaji huduma ya damu.
Aidha,
Ummy alisema kuwa asilimia 50 ya wanaotumia madawa ya kulevya kwa
kujidunga sindano wana maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini hivyo
amewataka watanzania kutojihususha na matumizi hayo na kuepuka ngono
zembe.
Hata
hivyo, Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamad Bakari
Kambi alisema kuwa virusi vikubwa vya ugonjwa wa ini ni A,B na C ambapo
vimelea A huletwa na mtu asiye na maambukizi kula chakula kisicho salama
na kunnywa maji yasiyo salama.
0 comments:
Post a Comment