METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 13, 2017

MKUU WA WILAYA ARUMERU ALEXENDER MNYETI AKAMATA GUNIA ZAIDI YA MIA TANO KWENYE MSAKO WA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI KIJIJI CHA LENGOLONGI

Mkuu Wa Wilaya Ya Arumeru Ndugu Alexander Mnyeti Jana Tarehe 12.07.2017 Katika Msako (Operations) Ya Tokomeza Madawa Ya Kulevya Amewezesha Ukamataji Wa Takribani Gunia Mia Tano (500) Katika Kijiji Cha Lengolongi Mpakani Mwa Wilaya Ya Arumeru Na Monduli Zilizopatikana Kwenye Nyumba Takribani Kumi Na Mbili (12) Zilizokuwa Zimeandaliwa Kwa Minajili Ya Kuuzwa Ndani Ya Nchi Na Kusafirishwa Nje Ya Nchi.

DC Mnyeti Toka Ameanzisha Vita Ya Tokomeza Madawa Ya kulevya Hapa Wilayani Arumeru Amewezesha Ukamataji Wa Dawa Za kulevya Aina Ya Bangi Kwenye Vijiji Vingi Na Kutokomeza Mtandao Wa Mkubwa Wa Kihalifu Sugu Uliokuwa Unaratibu Ulimaji, Usambazaji Na Uzwaji Wa Bangi Kwa Baadhi Ya Watuhumiwa Kukamatwa Na Kufikishwa Kwenye Vyombo Vya Sheria Kujibu Mastaka Yanayowakabili.

Mosi Katika Msako Wa Jana Wa Madawa Ya kulevya Kwenye Kijiji Hichi Cha Lengolongi Mmoja Wa Watuhumiwa Ni Balozi Wa Eneo Hilo Anayejulikana Kwa Majina Ya Mungaya S.O Laanoi Ambaye Ndani Ya Nyumba Yake Yalipatikana Magunia 31 Ambapo Mtuhumiwa Na Wenzake Inaonyesha Ni Wakulima Wazoefu Wa Madawa Ya kulevya Aina Ya Bangi Na Watafikishwa Mahakamani Baada Ya Uchunguzi Kukamilika.

Aghalabu Siku Hii Ya Ya Jana Kwenye Msako DC Mnyeti Katika Kata Ya Mwandeti Tarafa Ya Muklat Watu Wanne Walikamatwa Na Magunia Kumi Ya Bangi Na Madebe Ya Mbegu Ambapo Uchunguzi Unaonyesha Pia Watuhumiwa Ni Wakulima Sugu Wa Bangi Ambao Majina Yao Ni Kakoi D. O Lomey Mwenye Miaka 48, Kadogo D. O Lominyaki, Ndomon D. O Lomey Na Nakuyati S.O Langusi Wote Wametiwa Nguvuni Na Vyombo Vya Usalama.

Mathalani Wakitoa Pongezi Nyingi Sana Kwa Mkuu Wa Wilaya Ndugu Mnyeti Wananchi Wa Vijiji Vya Lengolongi Na Ngaraoni Wametaka Msako Huu Uendelee Kama Alivyo Ada Ya Adhma Ya Dhamira Njema Ya Dhati Ya Kutokomeza Madawa Ya kulevya Kwenye Vijiji Vyao Kwani Limekuwa Tatizo Sugu Miaka Nenda Rudi Lakini Toka DC Mnyeti Ameteuliwa Na Mh. Rais John Pombe Magufuli Kilimo Hicho Kimeanza Kupotea Na Kitakwisha Kabisa Wilayani Hapo Kwa Uhodari Na Utendaji Mzuri Sana Wa Mkuu Wa Wilaya Kwa Ushirikiano Kuntu Na Wasaidizi Wake, Kwa Mantiki Hiyo Wanamuombea Kwa Mungu Azidi Kumlinda Na Kumpa Afya Njema DC Mnyeti Ili Aweze Kutumikia Majukumu Yake Vizuri Na Kwa Weledi.

Akihitimisha Mkuu Wa Wilaya Ndugu Mnyeti Amewataka Wale Wote Wanaoendeleza Kilimo Cha Madawa Ya kulevya Aina Ya Bangi Ndani Ya Wilaya Yake Na Mkoa Wa Arusha Wasitishe Mara Moja Kilimo Hicho Kwani Hatolala Mpaka Hakikishe Hakuna Kilimo tena Cha Bangi Ndani Ya Wilaya Yake Na Kutoa Nasaha Kwa Wananchi Kutoa Ushirikiano Kwake Na Kwa Vyombo Vya Usalama Ili kuwabaini Wale Wote Wanaokaidi Amri Ya Rais John Pombe Kupambana na Madawa Ya Kulevya Hususani Kilimo Cha Bangi Ya Kwamba Serikali Ina Mkono Mrefu Sana Wasitishe Mara Moja.

 Napenda Kuambatanisha Baadhi Ya Picha Za Msako Wa Madawa Ya kulevya Aina Ya Bangi Chini Ya Dc Mnyeti Ambapo Bangi Ilichomwa Hapo Hapo Na Baadhi Kuchukuliwa polisi Kama Ushahidi Wa Kimahakama.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com