Jeshi
la polisi nchini Malawi limesema kuwa limepewa kibali maalum cha
kumkamata Rais wa zamani wa nchi hiyo, Joyce Banda kwa tuhuma za
matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji fedha.
Jeshi
hilo limeeleza kuwa limekusanya vielelezo vya kutosha vinavyoonesha
kuwa Rais huyo wa zamani ni mhusika katika kashfa kubwa ya rushwa na
utakatishaji fedha kiasi cha dola za kimarekani milioni mia mbili na
hamsini ($250m), katika kashfa inayofahamika kwa jina la ‘cashgate
scandal’.
“Jeshi
la polisi la Malawi linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa kitengo chake
cha kupambana na rushwa na udanganyifu kimefanya uchunguzi kuhusu
tuhuma dhidi ya Rais Mstaafu, Joyce Banda na kimepata vielelezo vya
kuaminika,” imeeleza sehemu ya taarifa ya polisi kwa umma.
“Vielelezo
vilivyokusanywa vinaweza kuonesha kuwa Rais Mstaafu alifanya makosa
yanayohusu matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji fedha,” aliongeza.
Mama
Banda yuko nje ya nchi hiyo lakini polisi wamesema kuwa watatumia mfumo
wa polisi wa kimataifa (Interpol) kusaidia kumrejesha nyumbani ili
ajibu tuhuma hizo dhidi yake.
‘cashgate scandal’ ni kashfa kubwa ya rushwa kuwahi kutokea katika historia ya Malawi inayohusisha vigogo wa serikali.
0 comments:
Post a Comment