Majadiliano
kati ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli na wawakilishi
kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini
yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo nchini yameanza leo, Julai 31
jijini Dar es Salaam.
Taarifa
ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema
kamati ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa
Palamagamba Kabudi.
Imesema kamati kutoka Barrick inaongozwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu, Richard Williams.
Profesa
Kabudi amekaririwa katika taarifa hiyo akisema wamejipanga vizuri
kujadiliana na Barrick juu ya madai ya Tanzania katika biashara ya
madini ya kampuni hiyo nchini na itahakikisha inasimamia masilahi ya
nchi ipasavyo.
Williams imeelezwa ameshukuru uwepo wa majadiliano
hayo, akisema Barrick imepokea madai ya Tanzania kwa mtazamo chanya na
ipo tayari kujadiliana na kufikia makubaliano yenye masilahi kwa pande
zote mbili.
Rais aliunda kamati hiyo baada ya kupokea ripoti za
kamati zingine mbili, moja ilichunguza mchanga wa madini (makinikia) na
nyingine ya kitaalamu iliyochunguza masuala ya kisheria na kiuchumi
kuhusu mchanga huo unaosafirishwa nje ya nchi.
Monday, July 31, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Na Hamis Hussein -SINGIDA Umoja wa machifu mkoa wa singida umewaomba wanaumoja huo kufanya zoezi la kuwasimika machifu wengine katika maene...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya...
-
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) aki...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment