Kaimu
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Fred Matiangi, ametangaza amri ya
kutotembea usiku kwa miezi mitatu katika County za Lamu, Tana River na
Garissa ambazo zimekuwa zikishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Al
– Shaabab.
Amri
hiyo imetangazwa baada ya Bw. Matiangi kukutana na Rais Uhuru Kenyatta
wakati wa kikao cha Baraza la Taifa la Usalama la nchi hiyo.
Amri
hiyo itaanza kutekelezwa mara moja kuanzia saa 12:30 jioni mpaka saa
12:30 asubuhi katika County hizo tatu na maeneo ya jirani ambayo
yanaonekana kuwa hatari.
Hata hivyo, Bw, Matiangi, amesema amri hiyo haitahusu visiwa vya Lamu, Manda na Pate.
Ijumaa
ya wiki jana usiku, watu tisa waliuwawa kwa kuchinjwa na wanamgambo wa
Al – Shaabab katika vijiji vya Jima na Poromoko katika County ya Lamu,
ambapo siku ya Jumatano wanamgambo hao walivamia kituo cha polisi na
kuwaua maafisa watatu.
0 comments:
Post a Comment