Ofisa Mradi wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’
kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), Suzan Sita (kulia), akitoa
mada katika Warsha ya Siku tatu ya kuwajengea uwezo viongozi wa Umoja wa
Wanawake Masokoni iliyohusu ukatili dhidi ya wanawake na haki zao
iliyoandaliwa na shirika hilo inayoendelea katika Hoteli ya Lamada Ilala
jijini Dar es Salaam jana.
Viongozi hao wakiwa katika warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Warsha hiyo. Kulia ni Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Irene Daniel.
Taswira katika ukumbi wa mikutano.
Mwezeshaji Sheria wa Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa akichangia mada.
Mwezeshaji Sheria katika Soko la Ilala
Mchikichini, Consolata Cleophas, akichangia mada. (kulia) ni Mwezeshaji
Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Aisha Juma na kushoto ni Verdiana
Gervas kutoka Soko la Ilala.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Ilala Mchikichini, Bupe George akichangia mada.
Mwezeshaji Sheria wa Soko la Kigogo Kisambusa, Mariam Rashid akichangi mada.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wafanyabiashara masokoni Tanzania, Betty Mtewele akichangia jambo.
Mfanyabiashara kutoka Soko la Gongolamboto, Elika Mwakyusa akichangia.
Mwezeshaji Sheria katika Soko la Temeke Sterio, Johanitha Katunzi akichangia mada.
Mshiriki wa warsha hiyo akichangia jambo.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Aisha Juma akichangia jambo.
VIONGOZI Wanawake katika masoko jijini
Dar es Salaam wamemuomba Rais Dk.John Magufuli atembelee masoko
wanayofanyia shughuli zao ili aone changamoto ya miundombinu katika
masoko hayo.
Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam jana
na Mwezeshaji wa Sheria katika Soko la Ilala Mchikichini, Consolata
Cleophas wakati akichangia mada kwenye warsha ya siku tatu ya
kuwajengea uwezo viongozi wa umoja wa wanawake masokoni iliyohusu
ukatili dhidi ya wanawake na haki zao iliyoandaliwa na Shirika la
Equality for Growth (EfG)
Alisema wafanyabiashara wakiwemo
wanawake wamekuwa wakilipa ushuru kila siku katika masoko hayo lakini
manispaa husika zimeshindwa kuwajengea miundombinu kama vyoo bora, umeme
na maji hivyo kuwa changamoto kubwa kwao.
“Tumekuwa tukitoswa ushuru wa shilingi
500 kwa siku kwa kila mfanyabiashara lakini hatuoni jitihada zozote
zinazochuliwa na hizi manispaa zetu za kutuwekea miundombinu bora ndio
maana tunamupomba Rais wetu afanye ziara katika masoko tunayofanyia kazi
ili tuzungumze naye na kuiona changamoto hii tuliyonayo” alisema
Cleophas.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake
wafanyabiashara masokoni Tanzania, Betty Mtewele alisema wakati ufike
manispaa ziweke wazi sheria ya ulipaji wa ushuru kwa mfanyabiashara
ambaye hakufika sokoni kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na kuumwa
kwani anapo pona na kurudi katika eneo lake la kazi anatakiwa kulipa
ushuru wa muda huo wote ambao hakufanya biashara wakati alipokuwa
akijiuguza.
“Tunaomba manispaa zetu ziweke wazi jambo hili kwani limekuwa ni changamoto kubwa sana kwetu” alisema Mtewele.
Mwezeshai wa Sheria katika Soko la
Kigogo Sambusa Mariam Rashid alisema zabuni za uzoaji taka katika masoko
zinapaswa kuangaliwa kwa karibu kwani wengi wanaozipata hawana uwezo wa
kufanya kazi hiyo hivyo kusababisha masoko mengi kuwa na changamoto ya
mlundikano wa takataka ambapo alishauri kuondoa mfumo dume katika masoko
unaotoa tenda hizo na badala yake zitolewe fursa kwa wanawake ili
waweze kuingia katika kamati za masoko ili nao waweze kuchangia katika
mambo mbalimbali.
Elika Mwakyusa aliomba manispaa ya Ilala
kutenga eneo la soko Gongolamboto ambako hakuna soko kwani eneo
wanalofanyia biashara zao ni la mtu binafsi hivyo wamekuwa na changamoto
kubwa ikiwemo kumlipa ushuru mkubwa mtu huyo.
Mwezeshaji sheria wa Soko la Vingunguti
wa Simba, Maimuna Mungi alisema ushirikishwaji wa wanawake katika
maamuzi mbalimbali katika soko hilo hakuna kutokana na kuwepo kwa mfumo
dume jambo ambalo limechangia wanawake wafanyabiashara katika soko hilo
kushindwa kuzipatia kusaidiwa changamoto walizonazo.
Mwezeshai Sheria kutoka Soko la Temeke
Sterio, Batuli Mkumbukwa aliomba asilimia 10 ya fedha za makusanyo ya
ushuru zibaki katika masoko husika ili zisaidie ujenzi wa miundombinu.
Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi
kutoka EfG Suzan Sitha alisema lengo la warsha hiyo ni kuwaongezea
uelewa viongozi wanawake masokoni kuhusu ukatili dhidi yao pamoja na
kupanga mikakati ya kuendeleza kampeni za kupunguza ukatili dhidi ya
wanawake masokoni baada ya mradi kuisha.
Alitaja lengo lingine ni kutambua haki
za wanawake na wahanga wa ukatili dhidi ya wanawake pamoja na
kuwakumbusha viongozi juu ya wajibu wao na utunzaji wa kumbukumbu za
vikundi.
Sitha alisema warsha hiyo
imewashirikisha viongozi wanawake kutoka masoko ya Manispaa ya Ilala na
Temeke jijini Dar es Salaam, ambayo ni Ilala Boma, Gongolamboto,
Mombasa, Kiwalani, Mchikichini, Kigogo Fresh, Kigogo Sambusa, Chamazi,
Kiustu, Kinyerezi, Feri, Temeke Sterio, Buguruni, Gezaulole, Tabata
Muslim na Vingunguti kwa Simba.
Alisema karibu changamoto zote zilizopo
katika masoko zinalingana kubwa ikiwa ni miundombinu mibovu licha ya
wafanyabiashara kulipa ushuru na kuwa mradi huo wa Mpe Riziki Si Matusi
upo katika Wilaya ya Temeke na Ilala jijini Dar es Salaam ambapo mradi
mkubwa wa Sauti ya Mwanamke Sokoni upo katika mikoa tisa hapa nchini.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
0 comments:
Post a Comment