Kalamu ya; Beatrice Condrad
Maneno kutoka Kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa ndg, Humphrey Polepole
Ccm ambayo Msingi wake ni kufanya chama hichi kuwa chama cha Wanachama, maana yake ni Chama cha watu ,chama cha wanachama maanayake ni chama ambacho wanauma wa wanachama wanasema nini kifanyike nini chama kitende, uma wa wanachama una mwelekeo wa Sera zetu za chama, uma wa wanachama unaamua nini yale maelekezo ya chama Kwa serikali wananchi walikipa chama hichi dhamana ya kuongoza hili si jambo rahisi
Njiani huku tutakutana na marafiki ambao hawataki kufata sheria, njiani huku tutakutana na ndugu ambao WASULUMATI njiani huku tutakutana na vikundi na magenge ya watu ambao hayapendi kuona Nchi yetu inasimama katika Mwelekeo huu nchi ambayo wananchi wanapaswa kulipa kodi ili serikali iweze kuhudumia wananchi wake tutakutana na hawa watu wote na hawatafurahi tukiwaambia sasa munapaswa kwenda katika namna ambayo watu wa Taifa letu wanataka kujikana nafsi
Tunataka kuwakataa baadhi ya marafiki mienendo na tabia yao haviendani kabisa na kasi inayoendelea kwenye nchi yetu ,mageuzi ambayo Chama Cha Mapinduzi kinafanya, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Dk John Pombe Joseph Maguful ndg, yetu yeye ndiye amejitosa, amejitoa katika maisha yake katika kurudisha nchi yetu katika misingi iliyo imara, nchi hii inaporudi katika misingi nidhamu ya Chama nidhamu ya serikali utumishi namna ya kukusanya Mapato, namna tunatoa huduma za afya, tunagawana utajiri wa Taifa hili Kwa haki ni Kazi kubwa.Tunaamini na tumekwisha Amini na ndiyo maana tukafanya maamuzi, mageuzi hayo yatakuwa na faida na tija kubwa kabisa Kwa uma wa wanachama Chama cha Mapinduzi lakini uma wa wananchi wa Wananchi wa Taifa letu la Tanzania
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
0 comments:
Post a Comment