METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 3, 2017

UNAHITAJI UWEZO MZURI WA KUONA WAKATI UNAENDESHA CHOMBO CHA MOTO

Muhammad Shaban (Aluta.D) akimkabidhi vipeperushi alivyoandaa kwa kushirikiana na Kikosi cha Usalama Barabarani vinavyohusu Usalama Barabarani kwa Watoto  kwa DCP Mohammed Mpinga, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani

Na Muhammad Shaban (Aluta.D) na Emmanuel Furahini

Wahanga wanasema ‘mwenye macho haambiwi tazama’ yaani kama una macho huwezi ukaambiwa kuangalia kitu bali unatakiwa uangalie mwenyewe. Msemo huu unaweza kutumika wakati wakuendesha chombo chochote cha moto kwani unatakiwa uangalie unapokwenda kwa uangalifu, umakini na kwa tahadhari mara zote ili uendeshe salama.

KWANINI UNAHITAJI UWEZO MZURI WA KUONA WAKATI UNAENDESHA?

Tunapoongelea suala la kuendesha chombo cha moto, ni macho ndiyo yanatumika zaidi kuliko hisia zingine za mwili. Macho yanatumika kila wakati unapohitaji kuangalia vitu vilivyo mbele moja kwa moja, kujihadhari na vihatarishi kwa mfano, mashimo, pikipiki zinazotoka pembeni ghafla lakini pia kujaribu kukinga na taa za gari ya mbele au mng’ao utokanalo na jua linalozama.

Macho pia hutumika kuangalia taa za kuongozea magari na watu wanaotaka kuvuka njia pamoja na kuangalia magari mengine unazopishana nazo. Uono mzuri na makini, pamoja na usikivu ni muhimu kwa kuendesha salama.

Unahitaji kuona vizuri nini kinakuja, wakati huo huo unakuwa na mchakato wa kuangaliavihatarishi kutoka pembeni, na kuchuja (scan) vioo vyako vya pembeni na ya kuangalia nyuma. Unahitaji uwezo mzuri wa kuona (visual acuity) ili uweze kuona vyema mbeleunakokwenda, kama kuangalia watembea kwa miguu na vihatarishi vingine.

Vilevile unahitaji kuwa na uwezo mzuri wa kuona pembeni (visual fields) uonaji wako wa pembeni kwa kawaida ni mzuri kugundua mienendo ya eneo pana kuelekea kwako. Uonaji huu wa pembeni ni muhimu, kwa sababu unahitaji kuona kitu chochote kwa haraka (magari, watembea kwa miguun.k.) vinavyokuja kwako kutoka pembeni. Kama unaendesha kwa mwendo wa kasi unaweza kufanya kutoweza kutumia vioo vya pembeni ipasavyo kitu ambacho kinaweza kusababisha ukakaribia hatari kubwa bila kuigundua.

Hivyo basi, dereva anapoendesha chombo cha moto hupata taarifa nyingi zinazohitajika kwa kupitia macho kwahiyo uwezo mzuri wa kuona ni muhimu kwa uendeshaji salama na pale 
unapohitaji kuvaa miwani (spectacles) au lenzi za kubandika kwenye mboni (contact lenses) kuona, lazima uvivae wakati wote unapoendesha. Bila ya hali nzuri ya afya macho na uwezo mzuri wa kuona, uendeshaji wa chombo cha moto inaweza sio hatarishi kwa mtumiaji tu wa chombo hicho na abiria wake bali kwa watumiaji wengine wa barabara pia.

SHERIA INASEMAJE

Notisi ya Serikali namba 31 ya 30/01/2015 (Government Notice no.31 on 30/01/2015) sehemu ya 4 (4) inasema “Where the driver under sub-regulation (2) and (3) intends to appear for a test, he shall before such appearance, obtain and produce a medical examination report of � his fitness for driving a motor vehicle from a recognized medical facility”

Hii inamaana kwamba kabla ya kuancha mchakato wa kupata leseni ya udereva, ni lazima kupimwa afya na kuleta ripoti ya afya njema itakayokuruhusu kuendesha chombo cha moto.

Hii inajumuisha na afya ya macho pia na kupewa cheti. Unapaswa kupimwa macho kutoka Hospitali ya serikali au inayotambulika kisheria kabla ya kwenda kutahiniwa mafunzo ya udereva kuomba leseni mara ya kwanza au tena iwapo imeisha muda wake.

Unahitaji kuvaa miwani ya lenzi za kubandika kwenye jicho (contact lenses) kila mara unapoendesha chombo cha moto iwapo unashida ya kuona.

NINI YAHITAJIKA KISHERIA KUONA VIZURI ILI KURUHUSIWA KUENDESHA?

Uwezo mzuri wa kuona ni muhimu kuhakikisha uendeshaji salama wa chombo cha moto. Ni muhimu kuwa na uwezo mzuri wa kuona mbele na karibu (Visual Acuity) ili kutambua umbali ili kufanya maamuzi sahihi. Watumiaji wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo ili kuthibitika kupatiwa leseni kuendesha:

KUNDI LA KWANZA

Madereva wa Magari madogo, bajaji na pikipiki

Lazima uweze kusoma kibao cha namba za gari (kwa miwani au lenzi za mboni ikibidi) kutoka umbali wa kiasi cha mita 20 katika mwanga mzuri wa mchana.

Wanahitahi kuwa na uwezo wa kuona (visual acuity) ya angalau 6/9 kwenye jicho zuri (kwa miwani au lenzi ikibidi) na pia wanahitaji kuwa na uwezo mzuri wa kuona pembeni.

Magonjwa kama Glaukoma (Presha ya Macho) huathiri uwezo wa kuona pembeni(peripheral vision).

KUNDI LA PILI

Madereva wa Magari makubwa ikiwemo Lori na Mabasi ya kubeba abiria

Kundi hili wanahitaji kuwa na uwezo wa kuona (visual acuity) ya angalau 6/7.5 kwenye jicho bora na angalau 6/60 na kwenye jicho baya. Hapa pia ni muhimu kuwa na uwezo mzuri wa kuangalia pembeni (peripheral vision).

Kwa makundi yote, huwezi kuruhusiwa kuendesha iwapo una ona vitu wiviliwili (double �vision)

VIPIMO VYA MACHO

Vipimo vya macho hufanywa aidha na wataalmu wa Macho (Optometrist) au 
Ophthalmologist (Daktari Bingwa wa Macho) waliosajiliwa na itahusu:

a. Visual Acuity Testing – yaani kuangalia unaona kiasi gani kwa umbali kwa kutumia Chati ambayo huwekwa mita 6 kawaida na kuambiwa kusoma herufi ambazo zinapungua urefu ili kujua ni kiasi gani unaweza kuona.

b. Anatomical Structures – Kutazama hali ya macho ya upande wa nje na ndani kwa kutumia Tochi, Slit Lamp na Ophthalmoscope.

c. Visual Field Test – Kucheki uwezo wa kuona pembeni kwa njia zinazotambulika

d. Motility Test – Kucheki iwapo macho yanweza kusogea pande zote ili kuhakisha hakuna tatizo la kengeneza au kuona vitu viwiliwili.

e. Funduscopy – Kuangali ndani ya macho iwapo kuna shida ya kisukari au presha ya macho

f. Streopsis – Kucheki iwapo unaweza kutambua umbali wa vitu kwa usahihi

g. Ishihara Test – Kucheki iwapo unaweza kutambua rangi kwa kutumia kitabu maalum

kiitwacho Ishihara. Iwapo una tatizo la kuona rangi, unaweza kuruhusiwa kuendesha ila unatakiwa utambue matatizo amabzo unaweza kukutana nazo na kusababisha hatarishi kama kutambua alama za barabarani na taa za kuongozea magari.

JINSI YA KUTUMIA MACHO IPASAVYO

Kupata taarifa kupitia macho inajulikana kama visual mtazamo (visual perception). Uendeshaji salama unahitaji uwezo wako wakuangali vitu vingi kwa pamoja.

Ili kupata taarifa sahihi kwenda kwenye ubongo, madereva wanatakiwa kuyazungusha macho yao mara kwa mara na kutazama sehemu maalum kwa wakati maalum.

Macho yetu yana uwezo wa kuona:

* Mbele moja kwa moja (Central Vision)

Uwezo wetu wa kuona mbele ni digri 3 ya uwezo wote wa kuona na asilimia 97 ni ya kuona pembeni. Hii digri 3 ni sehemu ndogo sana kwenye uwezo wa kuona ila inatuwezesha kufanya maamuzi muhimu kama kutambua umbali na taarifa zilizopo mbele yetu.

* Pembeni (Peripheral Vision)

Hii sio kali kama ile ya kuangalia moja kwa moja, ila inatambua mwanga na mwendo. Hii ni muhimu kwasababu inatuwezesha kutambua mazingira ya pembeni yetu, hata kama tusipogeuka kuangalia pembeni. Kwa mfano, magari yanayokuja kutoka pembeni, vimulimuli kutoka magari za kubebea wagonjwa au zimamoto yote hayo yanaweza kuangaliwa kwa kupitia uwezo wa kuona pembeni.�

Uwezo wa kuona mbele na pembeni ndizo zinatengeneza uwezo wa kuona kwa ujumla (entire visual field), na hii ni chanzo muhimu kwa madereva kwa uendeshaji salama. Ajali na uzembe mwingi hutokea kwasababu ya kutotumia macho ipasavyo.

1. Tazama Mbele – Utazame mbele, sio chini (ingawa inabidi kupitisha na macho chini pia kuangalia walemavu, watoto au wanyama).

2. Tembeza macho yako – Tembeza macho yako kuangalia sehemu muhimu

3. Tazama kwa upana – Chunguza sehemu zote hasa kwa kutumia vioo vyako

MAMBO MENGINE MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOENDESHA

* Unapoendesha wakati wa jua kali au sehemu zinaponyesha barafu kunaweza kuwa na mngao.

Unaweza ku:

a. Kutumia Sun-Visor (kinga ya juu ya kushusha ndani ya gari ya kuzuia mwanga wa jua)

b. Miwani ya jua ya kupunguza mwanga na mngao yenye kinga kati ya 0-3.

c. Hata kama unatumia lenzi za mboni, ni vyema kutumia miwani ya jua au zenye kinga ya kuzuia mngao

d. Unaweza kutengeneza miwani zenye lenzi za kupunguza mwanga kutokana na mwanga wa jua

* Unaweza kutengeneza miwani za jua zenye namba pia

*Unaweza kutengeneza lenzi maalum ziitwazo ‘Anti-Reflection’ ambazo zinasaidia kupunguza mngao hasa unapoendesha muda wa usiku

* Hakikisha vioo vya chombo cha moto hasa za mbele na nyuma zipo safi na waipa inafanya kazi vizuri

* Ni muhimu kupimwa macho mara kwa mara (angalau miezi 6 au kila mwaka) na hakikisha miwani

yako ina namba ya sasa na sahihi
* Vaa miwani yako ya kuona mbali mara zote hata unapoendesha gari au miwani ya jua

* Ni vyema ukawa na miwani ya akiba kwenye gari hasa kama namba ya miwani yako ni kubwa

* Kama unausingizi, ni bora usiendeshe gari

* Kamwe usifumpe jicho au macho unapoendesha gari au kuangalia sehemu ambayo inaweza 
kusababisha ajali

* Kamwe usitumie kilevi au dawa za kulevya

* Vaa miwani ya kinga unapoendesha pikipiki

* Zingatia dawa zingine za macho zinaweza kusababisha kupungua kuona hivyo zingatia masharti ya 
dawa za matibabu iwapo zinakuruhusu kuendesha gari

* Usitumie dawa yeyote ya macho bila ruhusa ya mtaalamu na iwapo kuna vipimo unahitaji kufanyiwa 
zenye kuewekwa dawa, uliza iwapo utaweza kuendesha gari.

* Usiondoe kuangalia na macho barabarani wakati unaendesha kwa kuongea kwenye simu, kula au � kunywa, kuongea n.k.

Macho Makavu

Kiyoyozi na hita zinaweza kusababisha macho kuwa makavu. Hii inaweza kuwa mbaya zaidi iwapo macho yako yanatabia ya kuwaga makavu. Macho makavu husababisha muwasho na hivyo 
kusababisha macho kujaa machozi na inaweza kufanya uono hafifu. Zuia upepo wa kiyoyozi au hita isipige machoni moja kwa moja kwa muda mrefu.

Kuingiwa na kitu jichoni (Foreign body)

Hakikisha unavaa kinga ya macho unapoendesha pikipiki au gari iliyo wazi ili kuzuia kitu chochote kama vumbi kisiingie jichoni.

Iwapo kuna kitu kimeingia kwa bahati mbaya, weka chombo cha moto pembeni na simama. Funga na kufungua macho mara kwa mara. Hii itasababisha machozi kutoka, na inawezekana hicho kitu kikatoka chenyewe. Kama hii hakijaweza kukitoa, unaweza kunawa jicho na maji masafi mengi na iwapo hiyo pia hakijatoa basi wahi kuonana na  mtaalamu wa macho au idara za dharura (emergency departments) karibu yako kwa msaada wa dharura.

TUNZA MACHO YAKO

Kuwa na uwezo mzuri wa kuona na afya nzuri ya macho ni muhimu sana na yapaswa tuyatunze 
macho yetu na kuyatumia ipasavyo kuendesha salama.

Imetayarishwa na Muhammad Shaban (Aluta.D) na Emmanuel Furahini ambao ni wote ni wataalamu wa Macho (Optometrist). Shukrani za kipekee kwa Afande Deus Sokoni na Afande Daud Mtunguja wa Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani.

Kwa maoni wasiliana nasi kwa namba 0788102897.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com