METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, June 27, 2017

PICHA MACHINGA MWANZA WAKUBALIANA NA SERIKALI

Machinga Jijini Mwanza wameeleza kufurahishwa na mpango wa serikali kuwatambua rasmi na kuahidi kuwapatia vitambulisho maalumu kama wafanyabiashara ndogondogo.
Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga mkoani Mwanza Shiuma, Matondo Masanya, ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kupitishwa kwa bajeti kuu ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2017/18 bungeni mjini dodoma.
Katika bajeti hiyo yenye makadilio ya shilingi Tirioni 31.7, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alieleza azima ya serikali kuwatambua machinga pamoja na mama ntilie nchini kwa kuwapatia vitambulisho maalumu ili serikali iweze kukusana kodi kutokana na shughuli za makundi hayo.
Kutokana na mkakati huo, Shirika la Shiuma lenye usajili wa kufanya shughuli zake kitaifa, limesema liko tayari kushirikiana na serikali kuanzia mchakato wa awali wa utengenezaji wa vitambulisho kwa ajili ya machinga ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com