Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu anawataarifu wakazi wa Wilaya hiyo kuwa Mwenge wa Uhuru unataraji kuwasili Katika Wilaya hiyo kesho Alhamisi June 29, 2017 katika Kijiji cha Mkiwa, Kata ya Mkiwa ukitokea katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Ukiwa Wilayani Ikungi Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Kilomita 77.9 ambapo utazuru Miradi yenye Jumla ya shilingi 2,417,184,466.72
Mhe Mtaturu amesema kuwa Jumla ya Miradi tisa itatembelewa na Mwenge wa Uhuru ambayo ni miradi ya Sekta ya elimu, Afya, kilimo, Maendeleo ya Jamii, Biashara, Viwanda na Utawala.
Miradi itakayozinduliwa ni pamoja na Programu ya Kilimo cha Korosho, Madarasa ya Shule ya Sekondari Mkiwa pamoja na matundu 10 ya vyoo vya shule hiyo.
Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg Amour Hamad Amour ataweka Jiwe la msingi ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Jiwe la msingi Zahanati ya Kijiji cha Ulyampiti sambamba na kugawa vyandarua ili kujikinga na Malaria na kuweka Jiwe la msingi kiwanda cha Mwananchi Cha kukamua Mafuta ya Alizeti sambamba na kufungua klabu ya wapinga Rushwa katika shule ya Sekondari Ikungi.
Mhe Mtaturu amesema kuwa Wilaya ya Ikungi inaunga mkono kauli mbiu ya mwaka huu 2017 ya Shiriki ukuzaji wa uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu.
Mkesha wa Mwenge wa Uhuru utakuwa katika viwanja vya shule ya Msingi Puma, Kijiji cha Puma ambapo pia utakapozuru katika Kijiji cha Puma utatembelea vikundi vya vijana na wanawake vya kiuchumi ambavyo vimewezeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kupitia mapato ya ndani, sambamba na Kuwapatia kadi za Bima ya Afya waathirika wa Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI.
Aidha, June 30, 2017 Mwenge wa Uhuru Utaelekea Manispaa ya Singida ambapo utakabidhiwa katika Kijiji cha Unyamikumbi.
0 comments:
Post a Comment