METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, June 25, 2017

MHE MIRAJI MTATURU APENDEKEZWA KUWA MLEZI WA BODI YA MFUKO WA ELIMU WILAYANI IKUNGI

Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekubali mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa elimu Wilayani humo kuwa mlezi wa Bodi hiyo kwa muktadha wa kusaidia kufikia malengo ya Kuwa na elimu Bora.

Mapendekezo hayo dhidi ya Mhe Miraji J. Mtaturu kuwa mlezi wa mfuko huo yametolewa na bodi ya mfuko wa Elimu wakati wa kikao cha pamoja na Dc Mtaturu  kupokea taarifa yao ya mkakati wa kupunguza ama kuondoka kabisa Changamoto za elimu katika Wilaya ya Ikungi.

Wazo la kuanzisha Mfuko wa Elimu lilitokana na kikao cha wadau wa elimu kilichoitishwa na Mkuu huyo wa Wilaya mwezi Disemba, 2016 na kubaini changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi kuanzia elimu ya msingi mpaka Sekondari.

Katika Kikao hicho kuliadhimiwa maazimio 43 ambayo yalizaa wazo la kuanzisha mfuko wa elimu ambapo wazo hilo lilifikishwa kwenye baraza la madiwani na kupokelewa kwa kauli moja ndipo mwezi Aprili mwaka 2017 baraza liliridhia kuanzishwa mfuko na kuteua wajumbe 15 wa bodi ya mfuko wa elimu wa Wilaya ya Ikungi.

Akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa Bodi ya elimu imebaini uwepo wa Changamoto mbalimbali ikiwemo Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.

Mhe Mtaturu alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto zote hizo Bodi imebainisha kuhitajika jumla ya fedha taslimu shilingi bilioni 28.

Hata hivyo Baada ya vikao mbalimbali vya maamuzi Bodi ya mfuko wa elimu imebainisha  mpango mkakati wa miaka mitatu kwa mtazamo wa Shule zenye hali mbaya zaidi hivyo kuandaa makadirio ya gharama za shilingi Bilioni 3.

Mhe Mtaturu alisema kuwa ili kufanikisha mpango huu kwa wakati husika Bodi imetoa mapendekezo ya wadau watakoombwa kuchangia mfuko ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi  kuchangia 3% ya mapato yake ya ndani.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko wa elimu Wilayani Ikungi Ndg Maulid Athuman akizungumza kwa niaba ya wajumbe wote amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kukubali kuwa mlezi wa Bodi kwani Bodi hiyo inaamini kuwa kwa dhamana hiyo atasaidia kutatua changamoto za elimu katika Wilaya hiyo.

Athumani alisema kuwa Wazo lililotolewa na Mkuu huyo wa Wilaya mwaka Jana la kuanzisha Bodi ya elimu ni matarajio ya kupatikana weledi katika elimu endapo Kama matazamia yote ya Bodi yatakamilika Kama ilivyokusudiwa.Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Elimu Wilayani Ikungi.Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Elimu Wilayani Ikungi.Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Elimu Wilayani Ikungi.Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko wa elimu Wilayani Ikungi Ndg Maulid AthumanMkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Elimu Wilayani Ikungi.Wajumbe wa Bodi ya Elimu Wilayani Ikungi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao kazi kuwasilishi mpango mkakati wa kuinua elimu Wilayani Ikungi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com