Mfalme
Salman wa Saudi Arabia amemchagua mwanae Mohammed bin Salman kuwa
mrithi wa kiti cha ufalme akimuondoa wadhifa huo binamu yake, Mohammed
bin Nayef.
Kwa
mujibu wa sheria ya nchi hiyo, mteule huyo pia anapata nafasi ya kuwa
Naibu Waziri Mkuu huku akiendelea na nafasi yake kama waziri wa ulinzi.
Aidha,
kwa muujibu wa kituo cha runinga cha nchi hiyo, mfalme huyo wamemvua
Pince Mohammed bin Nayef cheo cha kuwa mkuu wa mambo ya usalama wa ndani
ya nchi.
Mfalme
Salman mwenye umri wa miaka 81, alivikwa taji la ufalme wa Saudi Arabia
Januari 2015 baada ya kifo cha kaka yake, Abdullah bin Abdul Aziz.
Hatua
ya kuteuliwa kwa Prince Mohammed bin Salman mwenye umri wa miaka 31
kuwa mfalme ajaye kumeelezwa kuwa ishara ya mabadiliko makubwa kwa
kizazi cha vijana.
0 comments:
Post a Comment