METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, June 22, 2017

MD KAYOMBO ABAINISHA MPANGO MKAKATI JUU YA UKUSANYAJI MAPATO MWAKA 2017/2018

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akionyesha kipeperushi kinachotoa elimu ya Kodi wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba CCM
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba CCM Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba CCM Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba CCM Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amebainisha kuwa Manispaa ya Ubungo imejipanga vyema kukusanya mapato makubwa katika kipindi Cha Mwaka mpya wa Fedha 2017/2018.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kimbamba CCM, Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeanza kutoa elimu ya Kodi kwa wananchi  ikiwemo ugawaji wa  vipeperushi vyenye kufafanua kodi mbalimbali zinazotozwa na Manispaa zikiwemo zile za Sevice Levy, Leseni za vileo na Biashara.
Alisema kuwa tayari vipeperushi vimeanza kusambazwa katika Kata zote za Manispaa na sehemu mbalimbali zenye mikusanyiko ili watu waweze kupata elimu hiyo ya kodi.
"Ili kuonyesha umakini katika hili la elimu kuhusu kodi nanyi waandishi wa habari nitawagawia vipeperushi hivyo vya elimu ya kodi hi leo Ili mkawe mabalozi wazuri katika kuhabarisha Umma wa Watanzania" Alisema Kayombo.
Mkurugenzi kayombo alisema kuwa Manispaa ya Ubungo inatengeneza  mabango maalumu ambayo yatasimikwa maeneo mbalimbali yakielezea baadhi ya kodi zinazotozwa, sambamba na mpangp wa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwenye ukusanyaji wa mapato.
Sambamba na hayo pia Mkurugenzi Kayombo aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Manispaa hiyo imeanza kutoa mafunzo ya siku nne kwa Wenyeviti, na  Watendaji wa Kata na Mitaa ili kuwajengea  uelewa juu ya matumizi mazuri ya fedha ambazo zinapelekwa kwao katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Alisema kuwa Kwa bajeti  inayoisha kabla ya Mwezi wa saba zimepelekwa Bilioni 1.8 katika Kila  Kata kwa ajili ya kutengeneza Barabara zote ambazo ziliharibika kipindi cha Mvua na wasimamizi wakuu ni viongozi hao.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com