METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 26, 2017

MAFUNZO KWA VIJANA WA VYUO NA VYUO VIKUU CCM YAMALIZIKA HOMBOLO

Na: Mwandishi wetu, Dodoma

Wanafunzi kutoka vyuo 10 vya Mjini Dodoma  wamemaliza Kambi/Mafunzo ya siku tatu(3) yaliyotolewa  kwa Lengo la kuwaongezea Ufahamu juu ya Chama Cha Mapinduzi na Mambo mbalimbali yanayoendela hapa nchini.

Mafunzo hayo yaliyofunguliwa 23/06/2017 na Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole na kufungwa 25/06/2017 na Katibu wa NEC siasa na uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga yalihusisha wajumbe 551 wa Vyuo na Vyuo Vikuu vilivyopo katika Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza wakati wakati wa Kambi/Mafunzo hayo Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela alisema  Serikali ya Awamu ya tano(5) imejiandaa kikamilifu kikamilifu kupambana na Wezi wa mali za Umma.

"Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli imejipanga katika kuzuia mianya yote ya rushwa, nasisitiza kuwa hakuna mwizi atakayesalia katika ujenzi wa CCM Mpya na Tanzania mpya" Alisema Ndg. Lubinga

Pia akizungumza baada ya kufungwa mafunzo hayo Kaimu Katibu  wa Idara ya Vyuo na vyuo vikuu UVCCM Ndg. Daniel Zenda alisema kambi imeisha salama na vijana wameyapokea vizuri mafunzo hayo.

"Tunamshukuru mungu tumemaliza salama kambi/ mafunzo yetu na vijana wameyapokea vizuri na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote waliyofundishwa sambamba na kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kwa yale yote anayoyafanya" alisema Kaimu Katibu wa Vyuo na Vyuo Vikuu.

Pamoja na hatua  aliyochukua Rais Magufuli juu ya kuzuia  kusafirisha mchanga wa madini inapaswa kuungwa mkono na watanzania wote kwani pesa hizo zingesaidia kufanya shughuli nyingi za Maendeleo kama kuwezesha vijana kupata mikopo kupitia vikundi na Mikopo ya elimu ya juu, ujenzi wa Madarasa, Mabweni, Hospitali na Nyumba za walimu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo waliwataka wawe wazalendo kwa nchi yetu sambamba na kumuunga mkono Rais Magufuli kwa yale anayoyafanya ya kuwatetea wananchi wa Tanzania hususani Maskini na wanyonge. Dhamira na hatua anazochukua tunaziona kwa Vitendo ni dhahiri na ni shairi. "Maana Uzalendo ni Vitendo"

Wakati huo huo baada ya kumaliza mafunzo hayo Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lupinga aliweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Ofisi ya Vyuo na Vyuo Vikuu Tawi la Hombolo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com