Mji wa Khartoum, nchini Sudan.
Ndege ya kijeshi ya Sudan imeanguka Kaskazini mwa nchi hiyo na
kuwauwa wanajeshi wanne waliokuwa ndani. Mpaka sasa jeshi linabaini
kwamba ndege hiyo imeanguka kutokana na hali mbaya ya hewa.
Msemaji wa jeshi Brigedia Jenerali Ahmed Khalifa Shami amesema chanzo ajali hiyo ni hali mbaya ya hewa.
Mbali na hali mbaya ya hewa, makundi ya
waasi yamekuwa yakihusishwa sana na uangushaji wa ndege za kijeshi
katika maeneo yenye vita nchini humo.
Ajali kama hizo zimekua zikitokea nchini
Sudan, huku baadhi ya vyanzo vya usalama vikidai kuwa zimekua
zikisababishwa na hali mbaya ya hewa, wakati vyanzo vingine vikibaini
kwamba ndege nyingi nchini humo zimekua zikidunguliwa na makundi ya
waasi.
0 comments:
Post a Comment