METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, May 12, 2017

Waziri Mkuu Majaliwa kuongoza mkutano wa Tasnia ya Korosho

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu  wa Wadau wa Tasnia ya Korosho utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia  Jumamosi, Mei 13, 2007, mjini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho (CBT) Hassan Jarufu, amesema ya kuwa Mkutano huo Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Korosho utawajumuisha washiriki wapatao 600 na
utafanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango, Dodoma.

“Kama tulivyokwishakueleza, Mkutano huu Mkuu utafunguliwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa na watakuwapo pia Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi Dk. Charles Tizeba, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa inayolima Korosho ya Lindi, Pwani, Tanga, Mtwara na Ruvuma.

“Tumealika pia waheshimiwa Wabunge wanaotoka katika Mikoa hiyo, wakulima wa  Korosho na watendaji wa Vyama vya Ushirika vya zao la Korosho. Mkutano  huu utajadili kwa kina changamoto zinazoikabili Tasnia ya Korosho
nchini,” alisema Jarufu.

Mkutano huu Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Korosho unakuja katika wakati ambao Tasnia ya Korosho imepata mafanikio
muhimu katika msimu uliopita ambayo ni pamoja na kuweka udhibiti uliosababisha Korosho nyingi kuuzwa kwa kutumia mfumo wa Stakabadhi  Ghalani na hivyo kupunguza matumizi ya Kangomba, kipimo ambacho kwa muda
mrefu kimekuwa kikimnyonya mkulima. 









Udhibiti huo ulisababisha makusanyo ya Korosho kuongezeka kutoka tani 155, 244.645 msimu wa 2015/2016 hadi tani 264, 887. 527 katika msimu wa 2016/2017.

Kwa maelezo ya ziada  BOFYA HAPA
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com