Jumanne 16 May 2017
Leo tulikuwa na kikao cha watendaji wa UVCCM wa Kata zote kumi na nne (14) zinazounda Wilaya ya UBUNGO.
Tumekutana na kujadili mambo mbalimbali kwa ujenzi wa jumuiya zetu na kusimamia kanuni na miongozo inayotuongoza bila kuangalia dini, cheo, kabila wala sura ya mtu yeyote.
Kwa sasa tupo katika mchakato wa uchaguzi kwa hiyo tunapaswa kuwa makini, tutende haki, tushiriki kwa ukamilifu.
Pia wana UVCCM sikilizeni maelekezo ya viongozi wenu wa matawi yanayotoka Kata.
ANGALIZO
Kupanga uongozi (safu) ni kosa ambalo hatua zake hazitaangalia nani kapanga bali KANUNI YA MAADILI YA VIONGOZI ya 2012 itachukua nafasi yake.
Vijana ndio jeuri ya chama, sio kwa kukiuka kanuni na maadili tuliyojiwekea, bali kwa kukifanya chama kipate nguvu na uhai zaidi, sababu sisi tuna nguvu ya kufanya mambo mengi mazuri na kwa haraka.
Kauli mbiu, VIJANA TUKUTANE SITE
LEAH D. MBEKE
K/UVCM - UBUNGO
DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment