Mbunge
wa Mafinga Mjini Cosato Chumi ameitaka Serikali kusitisha mara moja
zuio la kulima vinyungu mpaka hapo tafsri ya umbali wa mita sitini
kutoka vyanzo vya maji itakafafanuliwa ipasavyo.
Akichangia
wakati Bunge limekaa kama Kamati kupitisha bajeti ya Wizara ya Maji na
Umwagiliaji , Chumi aliondoa shilingi na kuelezea kuwa suala la mita
sitini limetafsriwa tofauti na kuzua taharuki kwa Wananchi ambao baadhi
yao nyumba zao zimewekwa alama ya X.
'Mhe
Naibu Spika suala la kilimo cha Vinyungu ni suala la maisha kwa
Wananchi wa Mafinga, Mufindi, Kilolo, Njombe na mikoa ya Ruvuma na
Morogoro, na limekuwa likifanyika miaka nenda rudi na hakujawai kutokea
athari yoyote ya kimazingira"
Akiombwa
kuungwa mkono na Wabunge wenzake, Chumi alisema kuwa tafsri ya mita
sitini imekuwa ikitumika vibaya na kuwanyanyasa Wananchi ambao kilimo
cha vinyungu ni muhimu kwa maisha yao.
Wakichangia
hoja hiyo Wabunge wa Kilolo- Venance Mwamoto, Mbunge wa Mlimba- Suzan
Kiwanga, Mbunge wa Bunda -Mwita Getere, Mbunge wa Vwawa -Japhet Hasunga
na wa Kinondoni -Maulid Mtulia walisema kuwa hoja ya Chumi ni ya msingi
hivyo serikali isitishe mpaka hapo itakapothibitika mita sitini ni
kutoka umbali gani.
Akitilia
msisitizo katika hoja hiyo Mhe Mwamoto alisema kuwa ameuliza swali hilo
zaidi ya Mara tano lakini hakuna jibu la kueleweka kutoka Serializing.
'Kwanza wananchi hawajashirikishwa, pili hiyo njia mbadala mtakayowapa
ni ipi " aliuliza na kuongeza kuwa ni lazima serikali iwaambie wananchi
mita sitini ni kutoka wapi.
Mhe
Kiwanga alishangazwa na kinacjoitwa Kamati ya Bonde la Rubada na watu
wa Nemc ambao wamezua taharuki huko Kilombero kwa kuwatisha wananchi na
kuwataka waondoke kisa mita sitini.
"Kule
kwetu kila baada ya kilometa mbili unakutana na mto au kijito, na
maeneo ya vyanzo vya maji tunayatunza eti Leo ooh mita sitini hii sio
Sawa " alihoji Mbunge huyo wa Mlimba.
Akijibu
hoja hiyo, Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Lwaga
Mpina alisema kuwa suala la mita sitini ni la kisheria hata hivyo
Serikali iko tayari kwenda Mafinga ili kuona hali halisi na kufanya
tathmini.
"Inawezekana
hao wanaoweka x ni watu wa halmashauri au watu wa Nemc, hata hivyo
sheria kipengele cha 57 (2) kinatupa sisi nafasi ya kuangalia Hali
halisi na kupunguza hizo mita sitini, nmemuelewa Mhe Chumi, tutaenda
kuangalia tuone nini cha kufanya.
Waziri
wa Nchi Tamisemi George Simbachawene alifafanua kuwa ni kweli sio kila
vinyungu ni chanzo cha maji hata hivyo, ni vizuri Serikali ikapewa Muda
na kufanya tathmini.
"Kwa
kweli ni ngumu wananchi wale kukuelewa kuwazuia kulima vinyungu, kitu
cha muhimu kama alivyoeleza Waziri wa Mazingira, serikali tupewe Muda
tukatizame Hali halisi na kuona cha kufanya:
Kufuatia hoja hizo, Chumi aliitaka serikali kusitisha kwa muda mpaka hapo Naibu Waziri wa Mazingira atakapofanya ziara.
Lakini
pia alielezea masikitiko yake kuwa, pamoja na Waziri wa Maji Lwenge
kukiri kuwa Iringa ni mkoa unaotegemewa kwa vyanzo vya maji, Lakini
bajeti ya maji haizingatii hali hiyo na badala yake wamepewa bajeti
kiduchu.
Akizungumza
baadae na waandishi wa Habari, Chumi alisema kuwa amekuwa akipokea simu
na meseji za malalamiko kutoka kwa wananchi wa Mafinga wakieleza kuwa
wamezuiwa kulima vinyungu na baadhi yao nyumba zao zimewekwa X kwa madai
kuwa ziko ndani ya mita sitini kutoka mtoni.
"Kwa
kweli suala la kutuzuia kulima vinyungu hatuwezi kukubali kwa sababu ni
Sawa na kutukata mikono", aliongeza Mbunge huyo wa mafinga Mjini na
kusisitiza kuwa watu wa Mafinga na mkoa wa Iringa kwa ujumla wamekuwa
watunzaji wazuri wa vyanzo vya maji, iweje Leo wazuiwe kulima vinyungu,
kwa madai tu ya mita sitini.
Kilimo
cha vinyungu hulimwa wakati wa kiangazi kwenye maeneo ambayo ni ama ni
mabonde au yenye kuhifadhi unyevunyevu, na kimekuwa mkombozi wa
wanawake katika kunyanyua uchumi wao.
Ninaiomba
serikali isitishe suala hili ili kuondoa taharuki mpaka hapo tathimini
itakapofanyika, mana Wananchi wanaolima vinyungu sio vyanzo vya maji,
Ieleweke sio kila kwenye vinyungu ni chanzo cha maji:
0 comments:
Post a Comment