METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, May 29, 2017

MKURUGENZI MANISPAA YA UBUNGO AONGOZA WAKUU WA IDARA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo Mei 29, 2017 amewaongoza Wakuu wa Idara na Vitengo katika ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo ambayo itatembelewa na Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Ubungo.

Katika ukaguzi huo ikiwemo kutazama barabara itakayopitiwa na Msafara mzima Mkurugenzi Kayombo aliambatana pia na Afisa Utumishi mkuu Ndg Ally Juma Ally na Mchumi Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Ndg Yamo Wambura.

Akizungumza wakati wa Ukaguzi huo MD Kayombo amesema kuwa Miradi yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu zaidi ya shilingi Bilioni 2.8

Mwenge wa Uhuru unataraji kuzuru katika Manispaa ya Ubungo siku ya jumatano Tarehe 31, Mei 2017 ukitokea Manispaa ya Kinondoni.

Aliongeza kuwa, nchi nyingi zimekuwa kiuchumi kupitia viwanda na kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda, hivyo wananchi wanapaswa kuchangamkia fursa mbalimbali ili kufanikisha dhamira ya Serikali kufikia uchumi wa viwanda.

MD Kayombo alisema kuwa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 katika Manispaa ya Ubungo utapita katika Miradi mitano ya Maendeleo ambapo Miradi minne kati ya hiyo itazinduliwa na Mradi mmoja wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la Msingi.

Alisema kuwa maandalizi ya kuupokea Mwenge was Uhuru yamekamilika.

Imetolewa Na;
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com