Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kinondoni, SP Christopher Bageni akisindikizwa kupanda gari la askari baada ya kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Baada ya Mahakama ya Rufani kutoa hukumu dhidi ya vigogo wa polisi katika mauaji wafanyabiashara wa madini, familia ya mmoja wa marehemu amemuomba Rais John Magufuli kuwasaidia yatima walioachwa.
Akizungumza
jana, Martha Martine ambaye alikuwa mke wa marehemu Mathias Lunkombe
alisema kwa kuwa mahakama imeshatoa hukumu hiyo, hawezi kupingana nayo,
badala yake akaeleza namna kifo cha mumewe kilivyoiathiri familia,
hususan watoto wawili alioachiwa.
Katika
hukumu hiyo iliyotolewa juzi, aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya
jinai Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni alihukumiwa kunyongwa hadi
kufa huku Abdallah Zombe na wenzake wawili wakiachiwa huru.
Hukumu
hiyo ilitolewa baada ya rufani ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambaye
hakuridhishwa na hukumu ya Mahakama Kuu ambayo iliwaachia huru
washtakiwa hao.
Bageni
alikuwa ni miongoni mwa washtakiwa kwenye kesi hiyo iliyokuwa
inawakabili askari polisi tisa akiwamo Zombe ambaye alikuwa Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam.
Wafanyabiashara
Sabinus Chigumbi, ndugu yake Eprahim Chigumbi na Mathias Lunkombe na
dereva teksi, Juma Ndugu waliuawa Januari 14, 2006 kwenye Msitu wa Pande
uliopo Mbezi Luis, Dar es Salaam.
Kutokana
na hukumu hiyo, Martha alisema kwa sasa anaishi maisha magumu kwa kuwa
anatumia fedha nyingi kuwasomesha watoto wake Grace anayesoma kidato cha
nne na Fulmes anayesoma kidato cha pili.
Alisema
Serikali ilimuahidi kumsaidia kutunza watoto lakini hakuna msaada
wowote alioupata kutoka serikalini wala kwa kiongozi yeyote.
Kutokana
na hali hiyo, Martha alimwomba Rais Magufuli kuwasaidia watoto hao
kupata elimu na mahitaji mengine muhimu ili waweze kuja kujitegemea
kimaisha.
Mdogo
wa marehemu Protas, Mathias Lunkombe alisema tangu kaka yake
alipofariki amekuwa akihudumia familia mbili, ya kwake na ya marehemu
kaka yake.
Kuhusu
hukumu iliyotolewa, alisema haki imetendeka kwa kumhukumu Bageni
kunyongwa hadi kufa japokuwa hakuna hukumu ambayo ingeweza kupoza au
kuondoa machungu waliyonayo kwa ndugu yao aliyeuawa.
“Pamoja
na kumuua kaka yangu lakini kifo chake ni cha kumdhalilisha kwa sababu
walimsingizia kuwa ni jambazi ilhali ni mfanyabiashara wa madini. "
Mke wa Bageni asita
Wakati familia ya Lunkombe ikisema hayo, mke wa Bageni amekataa kuzungumzia hukumu kifo iliyotolewa kwa mumewe.
Mke wa Bageni asita
Wakati familia ya Lunkombe ikisema hayo, mke wa Bageni amekataa kuzungumzia hukumu kifo iliyotolewa kwa mumewe.
“Mimi
ni askari, nipo chini ya Kamishina (wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Simon) Sirro, siwezi kuongea na waandishi wa habari siruhusiwi kuongea
chochote,” alisema mke wa Bageni, Stella Saria na kuongeza:
“Kijeshi
sisi tuna miiko ya kazi, kama mume wangu amepata matatizo hayo ni mambo
ya kawaida, mimi nina viongozi wangu wa kazi, nilivyofundishwa kama ni
kitu cha familia yangu, Christopher alikuwa ofisa wa polisi watajibu
viongozi wake wapo.
“Mimi
nina amani ya kutosha, ni Mkristo nimempokea Yesu, tatizo haliwezi
kunitokea nikadharau miiko ya kazi. Mimi ni kiongozi askari, naelewa
miiko ya kazi lazima niiheshimu, samahani sana.”
0 comments:
Post a Comment