Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole
amelaani vikali kauli iliyotolewa na mtangulizi wake ambaye ni mbunge wa
jimbo la Mtama, Nape Nnauye kuwa alisaidia kukitoa chama hicho shimoni.
Nape
alitoa kauli hiyo dakika chache baada ya mkutano wake na waandishi wa
habari kuzuiwa na kutishiwa bastola na mtu mmoja, siku moja baada ya
kuondolewa kwenye nafasi ya Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo.
Polepole
alisema kuwa kauli hiyo ya Nape sio kauli sahihi ya kiongozi na kwamba
yeye pekee hawezi kukitoa chama shimoni huku kukiwa na wanachama milioni
nane na maelfu ya viongozi.
“Mwanachama
anayejitambua hawezi kusema anakibeba chama, wanachama wote milioni
nane walikuwa wapi? Viongozi wote maelfu walikuwa wapi? Nape ni kiongozi
wetu kwenye chama, kama kweli alisema maneno hayo alikengeuka sana,” Polepole anakaririwa na Mwananchi.
Katibu
huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM alisema kuwa Kamati ya Maadili
inapaswa kuliangalia suala hili na kumchukulia hatua Nape.
“Tuna
kila sababu za kumshauri Mzee Mangula wa Kamati ya maadili kuwa
hatuwezi kuwa na viongozi wa aina hii. Chama chenye watu milioni nane
unakitoa shimoni na nini? Unakitoa na ngazi, ulitumia kamba kukitupia
shimoni, uliita zimamoto? "Alihoji.
Hata
hivyo, Polepole alisema kuwa hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa viongozi
kama Nape sio za kuwawekea ukomo bali kuwalea kimaadili kwa kutumia
hekima na busara ili watambue kuwa chama sio punda anayeweza kutumbukia
shimoni.
Hivyo, alisema CCM iko kwenye mpango wa kuanzisha chuo kikuu kitakachotoa mafunzo kwa makada wake kuhusu nidhamu na maadili.
0 comments:
Post a Comment