METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, April 1, 2017

OFISI YA MKURUGENZI MANISPAA YA UBUNGO YATOA SEMINA ELEKEZI KWA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA

Watumishi wa kitengo cha sheria Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakiongozwa na Mwanasheria mkuu wa Manispaa hiyo Ndg. Merick Luvinga wametoa semina elekezi kwa wajumbe 150 wa mabaraza ya Kata kumi na nne (14) zilizopo ndani ya Manispaa hiyo.

Semina hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa  Manispaa ya Ubungo uliopo Kibamba CCM.

Semina hiyo iliyojumuisha wajumbe kutoka kata za Kibamba, Kwembe, Saranga, Mbezi, Mburahati, Manzese, Ubungo, Goba, Msigani, Kimara, Mabibo, Mburahati, Makuburi na Sinza ilikuwa na madhumuni yafuatayo;-

Kutoa mafunzo juu ya uwendeshaji wa mashauri ya ardhi( umiliki na mipaka), jinai, madai na migogoro ya ardhi katika katika mabaraza ya Kata zilizopo Manispaa ya Ubungo.

Kuwaelekeza wajumbe wa mabaraza juu ya taratibu za kufungua mashauri.

Kuwaelekeza wajumbe juu ya maadili na miiko yao.

Akizungumza wakati wa semina hiyo mmoja wa wajumbe wa  baraza kutoka Kata ya Kimara Bi. Betty Kombe alisema amefurahishwa na mafunzo hayo kwa kiasi kikubwa yamemjengea kujiamini na uelewa juu ya maswala ya kisheria.

Imetolewa na

Kitengo cha Uhusiano

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com