Waziri wa mambo ya nje wa Italia Angelino Alfano akizungumza wakati wa mkutano wa nchi za G7. April 11, 2017.
Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka nchi zilizoendelea kiviwanda G7
wameshindwa kukubaliana kuhusu kutangaza vikwazo vipya dhidi ya rais wa
Syria Bashar al-Assad au mshirika wake nchi ya Urusi, amesema waziri wa
mambo ya nje wa Itali Angelino Alfano.
Waziri Alfano amesema kuwa "kwa wakati
huu hakuna muafaka kuhusu vikwazo vipya kama njia sahihi," amesema
wakati wa mkutano wa siri wa siku mbili nchini Italia, baada ya waziri
wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson kuibua suala hilo kwenye
mkutano wao.
"Hakuna mawazo ya wazi yaliyotofauti,"
amesema Alfani ambaye ameongeza kuwa nchi za G7 zimesisitiza uungaji
mkono wao kuhusu vikwazo ambavyo vimewekwa kwa sasa.
Jumatatu ya wiki hii waziri Johnson
aliibua suala la kutangaza vikwazo zaidi kwa baadhi ya maofisa wa juu wa
jeshi la Syria na wale wa Urusi ambao wamekuwa wakishiriki kuratibu
operesheni za kijeshi.
Waziri wa fedha wa Marekani Steven
Mnuchin alisema wiki iliyopita kuwa Marekani hivi karibuni itatangaza
vikwazo zaidi kwa nchi ya Syria kama sehemu ya kijeshi, dipolomasia na
ufadhili wa fedha baada ya shambulio la silaha za kemikali.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa
Jean-Marc Ayraut amethibitisha waziri Johnson kuwasilisha wazo hilo hata
asubuhu ya Jumanne lakini nchi washirika hazikulijadili suala hilo kwa
kina.
Italia inasema inaamini vikwazo ni kama
chombo na sio kumaliza tatizo lililopo na kuonya kuhusu hatua ambazo
zitaitenga zaidi Urusi.
Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya
nje wa Marekani Rex Tillerson amesema rais Bashar al-Assad hapaswi kuwa
sehemu ya mustakabali ujao wa Syria.
0 comments:
Post a Comment