Wizara ya Kilimo imeanza utekelezaji wa hotuba yake iliyowasilishwa bungeni tarehe 24/25 Mei 2021 ikiwa na mtazamo chanya wa kuimarisha masoko na tija katika mazao.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda tarehe 27 Mei 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe maalumu kutoka Shirika la Chakula (WFP) Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Katika mkutano huo WFP imemuhakikishia Waziri wa Kilimo kuwa Shirika hilo litaendeleza ushirikiano maradufu baina yake na serikali ya Tanzania.
Akizungumza na Muwakilishi Mkazi wa WFP Bi Sarah Gordon Gibson amesema kuwa WFP imejipanga kuanza utekelezaji wa Miradi miwili kwa ajili kuwajengea uwezo wakulima wadogo katika mikoa ya Singida, Dodoma, Tabora na simiyu ikiwa ni njia mojawapo ya mkakati wa kuongeza tija.
Pamoja na mambo mengine Waziri Mkenda ameiomba WFP pamoja na mazao waliyokusudia katika utekelezaji wake pia waongeze na zao la alizeti katika mkakati huo ili kuimarisha soko la mafuta nchini.
Kadhalika, katika kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora nchini Waziri Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Wazalishaji wa Mbegu (TASTA) ili kuainisha changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Waziri Mkenda ameagiza watendaji wa Wizara ya Kilimo pamoja na TASTA kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya mbegu nchini.
Katika hotuba aliyoitoa Waziri Mkenda Bungeni Jijini Dodoma aliainisha kuwa serikali imejipanga Kufanya utafiti wa mbegu bora zenye tija.
Katika hatua nyingine ujumbe huo maalumu kutoka Shirika la Chakula (WFP) ukiongozwa na Muwakilishi Mkazi wa WFP Bi Sarah Gordon Gibson umekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment