METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, April 24, 2017

MAANDALIZI YA NANE NANE MANISPAA YA UBUNGO YAPAMBA MOTO


Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Mkurugenzi Ndg. John Lipesi Kayombo imeendelea kufanya maandalizi ya kutengeneza bustani katika eneo litakapojengwa banda la Manispaa hiyo litakalotumika katika maonesho ya sikukuu ya wakulima (NANE NANE).

Maandalizi hayo yameendelea jana kwa kusafisha na kupanda mazao ya aina mbalimbali katika bustani hiyo.

Mazao yaliyopandwa katika bustani hiyo ni mihogo, mipapai, viazi, passion, miembe, michungwa, vitunguu swaumu na vitunguu maji.

Maonesho hayo yanayotarajiwa kufikia kilele chake 8/8/2017 yatafanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere eneo la nane nane Kata ya Tungi Mkoa wa Morogoro.

KARIBU KATIKA BANDA LA HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO UJIONEE UTOFAUTI.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com