METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 18, 2017

FRIENDS OF BOYS WAKABIDHI ZAWADI

ALAWI HAIDAR FOUM
KATIBU FREINDS OF BOYS

Timu ya Friends of Boys wamekabidhi zawadi kwa mfungaji wa goli mechi ya Boys na Kipanga pia wamekabidhi zawadi za cheti kwa mchezaji bora wa mechi ya Boys na Kipanga.

Zawadi hizo ni muendelezo wa desturi ya Friends of Boys ya kutoa zawadi kwa mfungaji  na mchezaji bora mfungaji wa goli moja huwa anapewa alfu kumi (10,000) na atakaefunga magoli matatu mechi moja kwa maana ya Hat trick ana zawadiwa laki moja (100,000) na mchezaji bora anapewa alfu thalathini (30,000)

Siku ya leo Muharami Issa (MACERLO) alipata zawadi ya mchezaji bora na BARIQ Fii alipata zawadi ya Mfungaji.

Wachezaji wote kwa umoja wao walishukuru na kuitaka friends of boys kudumisha umoja wao maana tangu kuaza kutoa zawadi hizo motisha na moral wa wachezaji umeongezeaka wachezaji hao pia wameahidi kuendelea kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri uwanjani ili malengo ya timu kuchukuwa ubingwa yatimie.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com