Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tamisemi mhe,George Boniface Simbachawene
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais
anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George
Simbachawene amewaagiza maafisa utumishi kuwa waadilifu na wakweli
katika kutunza nyaraka zinazowahusu watumishi wenzao.
Aidha serikali inatambua kuwa
inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii na inajitahidi kulipa madeni hayo
inayodaiwa na mifuko ya Hifadhi za Jamii .
Simbachawene amesema hayo
wakati akifungua mkutano wa tisa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa niaba
ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Amesema baadhi ya maafisa
utumishi wamekuwa kama miungu watu na kupoteza nyaraka za watumishi huku
wanapobanwa na waajiriwa kuhusu taarifa za watumishi husema uongo
wakijua wenzao wanafamilia kama wao.
Pia amekemea tabia ya
watumishi wa masijala ambao wanapoteza kumbukumbu za watumishi kwa
makusudi hali inayosababisha baadhi yao kupunjwa madai yao kutokana na
baadhi ya kumbukumbu kupotezwa.
“Nawaomba nyie maafisa
utumishi muwe makini sana na maisha ya watumishi wenzenu oneni huruma
kwao mnapoteza kumbukumbu au kutoa ruhusa kwa watumishi Halafu mkibanwa
mnasema hamna taarifa hii inawaumiza watumishi wenzenu maana wanafamilia
zao kwanini muwafanyie mambo yasiyofaa mjirekebishe nyie pamoja na watu
wa masijala “.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya
Mfuko wa Lapf, Profesa Faustine amesema kuwa mfuko huo unajitahidi
kutoa huduma kwa wakati ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama na kubuni
mbinu za kukuza uchumi katika sekta ya viwanda.
Alisema mfuko huo utaendelea
kutoa huduma kwa wakati akiwemo fao la kulipwa jana kwa wanachama
wastaafu sanjari na kutoa mkopo wa maisha popote unaotolewa kwa
waajiriwa wapya kwakushirikiana na Benki ya CRDB.
Naye Mkurugenzi wa mfuko huo, Eliud
Sanga alishukuru wanachama hao kwa kushiriki katika mkutano huo sanjari
na kuuchagua mfuko huo ambao utatoa jana na hivi sasa wapo katika
uchambuzi wa Kiwanda cha chai cha Mponde, kilichopo Tanga, Kiwanda cha
Kuchataka nyama kilichopo Morogoro pamoja na kiwanda cha vifaa vya
hospitali Mkoani Shinyanga ambapo miradi hiyo itaanza kutekelezwa
mwishoni mwa mwaka huu
0 comments:
Post a Comment