Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema
akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika shule
katika viwanja vya Ngarenaro Jijini Arusha jana.

Wapili kutoka kushoto ni mbunge wa
Arusha mjini Godbless Lema ,wakwanza kulia ni mbunge wa Simanjiro James
OLemilya akifuatiwa na aliyeko kulia kwake ni Meya wa jiji la Arusha
Kalisti Lazaro,akifuatiwa na Wema Sepetu,na wakwanza kulia ni mwenyekiti
wa chadema mkoa wa Arusha Derick Magoma

Mbunge Lema akiwa na Wema Sepetu akisaliamia wananchi wa jiji la jana Arusha

Mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo jana jijini Arusha.
Na,Vero Ignatus ,Arusha
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan
Lema amefanya mkutano wake wa kwanza kwa kuzungumza na wananchi wa
Arusha baada ya kutoika rumande alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne
Akizungumza katika mkutano huo Lema
amesema kuwa madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema
watakao kuwa waoga yupo tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama
hawawezi kuwa majasiri waachanae na chama hicho.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa chama hicho wakiwemo madiwani wote wa chama hicho katika
jiji la Arusha pamoja na wabunge wa simanjiro na yule wa Monduli.
Aidha mbunge huyo amesema kuwa yupo
kwenye harakati za kukamisha kukiandika kitabu chake kitakachotoka hivi
karibuni chenye historia ya maisha halisi ya wafungwa waliopo gerezani
bila hatia,sambamba na wale waliobambikiziwa kesi mbalimbali.
Ameataka madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya .
0 comments:
Post a Comment