Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizungumza
na wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex alipofanya ziara kwa
ajili ya kusikiliza changamoto zao leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka
Kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana, Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la
Machinga Complex akielezea changamoto wanazokumbana nazo katika soko
hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene (hayupo pichani)
alipotembelea katika soko hilo leo Jijini Dar es Salaam. Waziri
Simbachawene amefanya ziara katika Soko hilo hili kusikiliza changamoto
kutoka kwa wafanyabiashara hao na kukagua utekelezaji wa agizo
alilolitao wakati wa ziara yake ya kwanza sokoni hapo mapema mwaka jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene (wapili
kutoka kushoto) akitembelea baadhi ya vizimba vya wafanyabiasha katika
soko la wafanyabiashara wadogowadogo la Machinga Complex leo Jijini Dar
es Salaam. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,
Meneja wa Soko hilo, na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia
Mmbando. Na: Mpiga Picha Wetu.
Na: Frank Shija – MAELEZO, Dar es Salaam
WAFANYABIASHARA ndogondogo katika Soko
la Machinga Complex Jijini Dar es Salaam wameshauriwa kubadilika na
kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria badala ya kufanya biashara
zao kimazoea.
Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George
Simbachawene alipofanyaa ziara ya kikazi katika Soko hilo ili kusikiliza
changamoto wanazokumbana nazo wafanyabiashara wa soko hilo.
“Nawapa pole sana ndugu zangu
wafanyabiashara wa Machinga Complex mnaendesha biashara zenu bila
kuzingatia sheria jambo linalo wagharimu hivi sasa katika biashara zenu
leo nimekuja kuwarejesha kwenye mstari,” alisema Simbachawene.
Aidha Waziri Simbachawene amemuagiza
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuwachukulia hatua baadhi ya
viongozi wa menejimenti ya Machinga Complex kwa kile kinachodaiwa
utendaji wao mbovu na kujaza nadfasi zote zilizo wazi,
Wakati huohuo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Paul Makonda kuteua Wajumbe wa Bodi ya Machinga Complex
ili kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa Soko hilo.
Pia Waziri Simbachawene ametoa wito kwa
wafanyabiashara wote kulipa kodi zao kwa wakati huku hakitishia
kuwaondoa katika vizimba (eneo la mraba la mauzo) wale wote watakao
kaidi amri hiyo halali ya kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na mikataba
yao.
Awali akimkaribisha Waziri Simbachawene,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa ujio wa Waziri
huyo mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa imekuja wakati muafaka kwani ni
takribani kipindi cha karibu mwaka mmoja tangu alipompa maagizo ya
kushughulikia changamoto zinazokabili jengo la Machinga Complex kazi
ambayo waliikamilisha na kukabidhi taarifa katika ofisi ya Waziri
Simbachawene.
“Nidhahiri kuwa ziara yako Mhe. Waziri
itatoa majawabu yatakayopelekea kutatua changamoto kadhaa zinazolikabili
soko hili la Machinga Complex na ni imani yangu kwamba utatoa maagizo
na kufanya maamuzi nasi hatuna budi ya kuyapokea na kutekeleza”
alisisitiza Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la
Dar es Salaam Bibi. Sipora Liana amesema kuwa changamoto kubwa
inayokabili Soko hilo ni pamoja na deni linalokadiriwa kufikia zaidi ya
shilingi bilioni 38 zianzodaiwa na Shirika la hifsdhi za Jamii (NSSF)
ambao ndiyo waliojengwa majengo ya soko hilo linalomilikiwa na
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine
inayokabili Soko hilo ni kutokuwapo kwa chombo cha maamuzi (Bodi) ambayo
kazi yake kubwa ingekuwa kushughulikia changamoto zote za mradi huo.
Soko la Machinga Complex limejengwa kwa
lengo la kutatua changamoto ya ukosekanaji wa soko la uhakika kwa
wafanyabiashara wadogowadogo katika Jiji la Dar es Salaam ambapo ujenzi
wake ulifanyika chini ya udhamini wa NSSF na kumilikiwa na Halmashauri
ya Jiji la Dar es Salaam likiwa na uwezo wa kuchukua takribani
wafanyabiashara 4206.
0 comments:
Post a Comment