METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 22, 2017

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KITAIFA YAENDELEA GOBA MANISPAA YA UBUNGO



Maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa yaliyoanza rasmi terehe 16/03/2017 yaliendelea jana Manispaa ya Ubungo kwa kupanda miti zaidi ya 70 katika chanzo cha maji kilichopo eneo la Matosa (Shule ya sekondari Matosa) katika Kata ya Goba.

Maadhimio hayo yenye kauli mbiu "Maji safi na Maji taka, punguza uchafuzi yatumike kwa ufanisi" yalianza rasmi tarehe 16/03/2017 kilele chake kinatarajiwa kuwa leo tarehe 22/03/2017 na mgeni rasmi ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda.

Dhumuni la maadhimisho hayo ni kuwafahamisha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika kupanga, kuendesha na matengenezo ya miradi ya maji pia kuimarisha usafi wa Mazingira kwenye vyanzo vya maji.

Imetolewa na Idara ya Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com