METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, March 14, 2017

Usalama Barabarani wajiimarisha kudhibiti ajali

JESHI la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani limesema limeongeza nguvu katika kusimamia sheria, kuboresha matumizi ya teknolojia na kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya barabara ili kukabiliana na ajali.

Limesema hatua hizo zimesaidia kupunguza matukio ya ajali nchini Kamanda wa Kikosi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga aliyasema Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kwa Mkutano Maalumu wa Kanda kujadili na kutathmini changamoto za usalama barabarani na jinsi ya kuzikabili.

“Mikakati tuliyo nayo sasa ni usimamizi wa sheria. Tumeendelea kuwa wakali kwa wanaovunja sheria, matumizi ya teknolojia katika usimamizi wa sheria kwa kulipa faini kwa njia ya kielektroniki, kudhibiti mwendo kasi na kutoa elimu kwa umma,” alisema.

Alisema, “Mwaka huu tutajipanua zaidi kwa kutumia teknolojia… Tuna mpango wa kuweka kamera zitakazokuwa zikipiga picha katika maeneo mbalimbali ili kuchukua hatua kudhibiti wanaovunja sheria.” “Tumelenga kupunguza ajali kwa asilimia 50 ifikapo 2020,” alisema.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com