Mtoto raia wa Syria akiwa kwenye mji wa Manbij, Machi 7, 2017
Unicef inasema kuwa, watoto 652
wamekufa, 255 kati yao waliawa wakiwa shuleni mwaka uliopita, ikiwa ni
ongezeko la asilimia 20 zaidi kutoka idadi ya waliokufa mwaka 2015.
Idadi hii inaelezwa kuwa ni ile idadi
ambayol imethibitishwa, hali hii ikimaanisha kuwa huenda idadi ikawa ni
zaidi ya inayotolewa sasa.
Shirika hilo linaamini kuwa watoto wanaofikia zaidi ya 800 walichukuliwa kwenda kujiunga na makundi ya wapiganaji mwaka 2016.
Ripoti inasema idadi hii ni mara mbili
ya ile ya mwaka 2015. Huku wale waliochukuliwa kwenda kupigana,
wakitumiwa kuwa mstari wa mbele na kutumiwa kama wauaji, walinzi wa
magereza na kujitoa muhanga.
Mkurugenzi wa Unicef kwa nchi za mashariki ya kati, Geert Cappelaere, anasema kuwa "ukubwa wa mateso wanayoyapata hauelezeki".
"Mamilioni ya watoto nchinik Syria
wanajikuta kwenye mashambulizi kila siku kutokana na vita vya wenyewe
kwa wenyewe, maisha yao hayaelezeki." amesema mkurugenzi huyo.
Watoto milioni 6 hivi sasa wanategemea
misaada ya kibinadamu kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, vita
ambayo sasa imedumu kwa zaidi ya miaka 6.
Watoto wanaokadiriwa kufikia milioni 2
na laki 3 wamekimbia nchi yao, huku walioko kwenye hatari zaidi
wakifikia milioni 2 na laki 8 na hawa wakiwa wamenaswa kwenye maeneo
yenye vita kali.RFI
0 comments:
Post a Comment