Mkurugenzi wa TBL Group na Rais mwa Masoko kanda ya Afrika Mashariki akitoa ufafanuzi katika warsha ya udhibiti wa bia haramu iliyoandaliwa na kampuni hiyo
Moja ya kipeperushi kinachoelezea ubora kwa kinywaji cha Chibuku
Watumiaji wa bia ya Chibuku wakifurahia baada ya kazi
TBL Group imekuwa mstari wa mbele kuwezesha wakulima kwa ajili ya kupata malighafi ikiwemo zabibu na Shahiri
–Chibuku na Balimi zazidi kukubalika kama bia za kitanzania na zilivyotengenezwa na malighafi yaTanzania
Wakati
tafiti zinabainisha kuwa bia zinazotengenezwa nchini Tanzania zinauzwa
kwa bei kubwa ambayo watumiaji wengi hawana uwezo wa kumudu
kuzinunua,kampuni ya TBL Group inaendeleza mkakati wake wa kuhakikikisha
inaimarisha masoko ya bia ya asili ya Chibuku ikiwemo kutengeneza bia
kwa kutumia malighafi zenye unafuu wa bei ili kuwezesha watumiaji wengi
kumudu kuzinunua.
Mkakati
huo ulibainishwa katika warsha ya siku moja kuhusu udhibiti wa pombe
haramu iliyoandaliwa na TBL Group jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
wadau mbalimbali wa sekta ya vinywaji na watendaji kutoka taasisi za
serikali liyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Wadau
kutoka sekta ya vinywaji walieleza bayana kuhusu changamoto kubwa
wanayokabiliana nayo katika soko ya kuuza bia kwa bei kubwa
zinazosababishwa na gharama kubwa za uzalishaji ikiwemo kodi kubwa
wanazotozwa kuanzia kwenye malighafi mpaka kwenye bidhaa.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin, ambaye pia ni Mkuu wa Masoko katika
ukanda wa Afrika Mashariki ,alisema kuwa kampuni yake imejizatiti
kutengeneza na kuimarisha soko la bia za gharama nafuu kama ambavyo
inaendelea kuwekeza katika bia ya asili ya Chibuku.
Alisema
kuwa bia ya Chibuku umaarufu wake umekuwa ukiongezeka siku hadi siku na
kutumiwa na wananchi wengi kutokana na kuwa na unafuu wa bei unaoendana
sambamba na vipato vya watanzania wengi na inatengenezwa katika
mazingira bora na kuwekwa kwenye vifungashio vya kisasa kulinganisha na
bia nyingine za asili ambazo zinapatikana katika mazingira yasio salama.
Utafiti uliofanywa na kampuni ya kimataifa ya utafiti wa matumizi ya bidhaa kwa walaji ya CanBack umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili unatawala soko la vinywaji vyenye kilevi Tanzania kwa asilimia 50%. “kutokana na ripoti ya utafiti huo wa kitaalamu,TBL Group imeboresha zaidi vinywaji vya asili aina ya Chibuku na Nzagamba vinavyotengenezwa
na viwanda vyake vya DarBrew ambapo vinapatikana kwenye chupa za ukubwa
wa aina mbalimbali kuwawezesha wateja kuvipata katika mazingira ya
usafi wakati huohuo kulingana na uwezo wa vipato vyao”Alisema.
Aliongeza kusema kuwa kupitia vinywaji hivi kampuni imeanzisha mpango unaojulikana kama ‘Chibuku Mamas’ wa kuwawezesha wanawake kuviuza na kujipatia mapato ambapo mpaka kufikia sasa unaendelea
kuwanufaisha Wanawake wengi kiuchumi wakati huohuo kulinda afya za
watumiaji wa pombe za asili waliokuwa wanatumia pombe zisizotengenezwa
katika mazingira salama “.Alisema Jarrin.
Wakati kampuni inayo mkakati wa kuimarisha masoko ya vinywaji vyake utafiti uliofanyika katika mabaa
mbalimbali jijini unabainisha kuwa mbali na bia ya asili ya Chibuku bia
zingine zinazouzwa kwa bei nafuu ikiwemo bia ya Balimi hivi zinazidi
kushika kasi kwa kuwa na watumiaji wengi ambapo pia wanazifurahia
kutokana na uasili wake wa kutengenezwa na malighafi ya mazao ya mtama na mahindi kutoka hapa nchini.
Bia
nyingine za TBL ambazo zinatamba kwenye soko nchini baadhi yake ni
Safari, Kilimanjaro, Ndovu, Castle Lager na Castle Lite .Kampuni pia
imekuwa kinara wa kutengeneza vinywaji vikali na mvinyo ambavyo navyo
vinatamba katika soko kwa asilimia 73% baadhi yake vikiwa ni – Konyagi za Chupa, Valeur za chupa na Dodoma Wine.
0 comments:
Post a Comment