Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya TCCIA
Investment PLC bi Magdalena Mkocha akizungumza na wafanyabiashara mkoani
Lindi katika ukumbi wa Double M humo.Bi Mkocha alisema TCCIA Investment
ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na mtaji wa shilingi Bilion 1.97 imeweza
kukuza mtaji hadi zaidi ya Bilion 28.6 na imekuwa ikilipa gawiwo kwa
wanahisa wakeMkochi ameongeza kuwa TCCIA Investment PLC ni kampuni ya
uwekezaji wa pamoja, imara na imekuwa ikifanya vizuri sana hivyo
amewahimiza wajasiriamali hao kuitumia fursa hii muhimu na adhimu kabla
ya March 14 mwaka 2017, ambapo milango ya uuzaji wa hisa hizo
itafungwa Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Chemba ya Biashara,viwanda na
kilimo, Magdalena Mkocha, amewataka wananchi na wafanyabiashara wa
Mikoa ya Lindi na Mtwara kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa ya
soko la hisa za TCCIA Investment PLC kwa awamu ya awali ambayo
inakaribia kuisha. Hayo ameyasema wakati akizungumza wafanyabiashara
kwenye ziara yake ya mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara alipokuwa kwenye
mikutano ya kuhamasisha ununuzi wa Hisa hizo ambazo zinamilikiwa na
kampuni hiyo.
Bi Magdalene Mkocha akifafanua jambo kwa
wafanyabiashara waliohudhulia mkutano huo mkoani Lindi “Nipende
kuwahimiza ndugu zangu tuchangamkie fursa hii kwasababu TCCIA Investment
PLC nikampuni imara ambayo imeweza kusimama na kujiendesha yenyewe kwa
kipindi kirefu bila kutegemea mikopo, sasa imeona ni wakati sasa kuwapa
na wananchi nafasi ya kushiriki katika kuchangia mitaji yao ili mwisho
wa siku wavune matunda kupitia hisa zao” alisema Bi Mkocha
Mmoja wa wajasiriali waliohudhulia
mkutano huo Bwana Condrad Makwiya akiuliza swali kwa bi Mkocha kuhusiana
na upatikanaji wa hisa hizo Hisa za TCCIA Investment PLC zinapatikana
kwa shilingi 400 tu, huku kima cha chini cha kununua hisa hizo kikiwa ni
hisa 100, pia unaweza kupata hisa hizo kupitia kwa mawakala wa
walioidhinishwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) au
tembelea kwenye matawi yoyte ya Benki ya CRDB. Pia unaweza kutumia simu
ya mkononi kwa kupiga *150*36# kisha kufuata maelekezo.
Bi Madgalena Mkocha akigawa vipeperushi
kwa wafanyabiasha mkoani Mtwara baada ya kumalizka kwa mkutano huo kulia
kwake ni Makamu Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Mtwara.
Moja ya mshiriki mkoni Lindi akitoa shukrani zake kwa uongozi wa TCCIA Investment PLC kuhusu fursa hiyo uuzaji wa hisa
0 comments:
Post a Comment