Aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Channel Ten mkoa wa Geita,Vallence Robert Amefariki dunia Hii Leo Tarehe 28/03/2017, akiwa nyumbani kwao Muleba Kagera. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake Ribarikiwe.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Geita Daniel Limbe amethibitisha taarifa za kifo cha mwandishi wa habari Valence Robert.
Limbe ameiambia Maduka online kuwa Valence Robert hivi karibuni aliondoka mkoani Geita akiwa anaumwa.
Hata hivyo inaelezwa kuwa Valence Robert alikuwa anaumwa ugonjwa usiojulikana. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo nyumbani kwao Misenyi.
Hivi karibuni Valence Robert na Joel Maduka walipigwa na askari polisi wakati wakiwatawanya wananchi kwenye maeneo ya stendi ya zamani Mjini Geita ambao walikusanyika kusalimiana na Waziri mkuu mstaafu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu Taifa ya Chadema Edward Lowassa.
0 comments:
Post a Comment