METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 29, 2017

Kikao cha wataalamu kutoka Korea Kusini chafana Dar es salaam

Kaimu Afisa Kilimo, umwagiliaji na ushirika wa Manispaa ya Ubungo Ndg. Salim Msuya akifuatilia kwa makini kikao hicho.
Timu ya wataalamu kutoka Korea Kusini na shirika la  maendeleo KOICA wakifuatilia kikao hicho.
Timu ya wataalamu kutoka Korea Kusini na shirika la  maendeleo KOICA wakifuatilia kikao hicho.

Na Nassir Bakari

Wataalamu wa kilimo, umwagiliaji na ushirika kutoka sekretarieti ya mkoa wa  Dar es Salaam, Halmashauri za Manispaa za mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Kaimu Afisa kilimo, umwagiliaji na ushirika Ndg. Salim Msuya kutoka Ubungo wakutana na kufanya kikao na timu ya wataalamu kutoka Korea Kusini na shirika la maendeleo la KOICA.

Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi mkubwa  wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Kikao hicho kilijadili mambo yafuatayo;-

Kuchochea maendeleo ya kilimo katika mkoa wa  Dar es Salaam.

Kuhamasisha maendeleo ya kilimo katika mkoa wa  Dar as Salaam.

Kuangalia maendeleo ya  kituo cha kilimo cha Malolo kilichopo Kata ya Mabwepande.

Kutoa mpango wa miaka mitatu (2017-2019) wa mafunzo kwa wakufunzi 15 (T.O.Ts) yatakayofanyika katika nchi ya Korea Kusini.

Pia kikao hicho kimekubaliana kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Wakuu wa wilaya , Wakurugenzi na waheshimiwa Madiwani wa Manispaa tano za mkoa wa Dar as Salaam watapata fursa ya kwenda Korea Kusini.

Kabla ya safari hiyo viongozi hao watapitishwa katika kituo cha mafunzo ya kilimo Malolo ili kupata uelewa wa pamoja.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com