Breaking news
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
amekamatwa na polisi akiwa nje ya Bunge mjini Dodoma leo.
Taarifa ya Chama chake cha Chadema imesema hakuna maelezo
yaliyotolewa kuhusu kukamatwa kwa kiongozi huyo.
Wakili wake Peter Kibatala amesema Askari polisi kadhaa
wakiongozwa na aliyetambuliwa kama mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Dodoma.
Hata hivyo wakili wake amedai kuwa mteja wake hakuonyeshwa
hati inayotoa amri akamatwe Wakili huyo amesema kuwa aliwasiliana naye mara
baada ya kukamatwa
Kabla hajakamatwa aliandika ujumbe huu na kuutuma
mtandaoni:
Ninawapa taarifa kwamba nimefuatwa nyumbani na askari wawili kutoka ofisi ya RPC Dodoma. Sijazungumza nao bado lakini ni wazi wana maagizo ya kunikamata na kunizuia kuja Arusha kwenye Uchaguzi wa TLS. Wameshindwa kuzuia uchaguzi wetu mahakamani…….
Wito wangu kwenu mawakili wa Tanzania:
Nendeni Arusha mkachague viongozi wa TLS watakaopigania haki za binadamu, utawala wa sheria na demokrasia. Msipofanya hivyo hakuna mtu yeyote, hata ninyi mawakili, atakayepona kwenye……..
Kumbuka, kama Nimrod Mkono anaweza kufungiwa ofisi na TRA ni wakili gani mwingine aliye salama???
Kama wakili anaweza kukamatwa mahakamani kwa kufanya kazi yake ya uwakili, ni nani miongoni mwetu aliye salama???
Nendeni mkapige kura kukataa mfumo wa aina hii.
Mimi naenda mahabusu, na pengine, gerezani. Nawaombeni kura zenu
0 comments:
Post a Comment