Shirika la mipango ya mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limeipongeza Kenya kwa kupiga marufuku uzalishaji, uagizaji na matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mkurugenzi mtendaji wa UNEP Bw Erik Solheim amesema hatua hiyo itaanza kutekelezwa mwezi Agosti na inatarajiwa kuhimiza wengine kuunga mkono kampeni ya kuwa na bahari safi.
Waziri wa mazingira na maliasili wa Kenya Bibi Judy Wakhungu ametangaza
amri hiyo ya serikali ambayo itaanza kutekelezwa ndani ya miezi sita.
Tangazo hilo limetolewa wakati Kenya inatumia mifuko ya plastiki ipatayo
milioni 100 kila siku, na kuleta changamoto kubwa kwenye uondoaji wa
taka za plastiki.
Wiki tatu zilizopita UNEP ilitangaza vita dhidi ya matumizi ya plastiki, kupitia mpango wake wa kusafisha bahari, na kusema serikali kumi zimeunga mkono mpango huo.
Wiki tatu zilizopita UNEP ilitangaza vita dhidi ya matumizi ya plastiki, kupitia mpango wake wa kusafisha bahari, na kusema serikali kumi zimeunga mkono mpango huo.
0 comments:
Post a Comment