Washambuliaji wa Boko Haram watekeleza shambulio
Ripoti kutoka kaskazini mwa Nigeria,
zasema kuwa watu waliokuwa na silaha na wanaoaminika kuwa wanamgambo wa
kundi la kiislamu la Boko Haram, wametekeleza shambulio katika mji wa
Magumeri.
Duru zasema kuwa waliwashambulia raia kiholela huku wakiteketeza majumba yao.
Kuna ripoti inayosema kuwa, moshi mkubwa unaonekana ukifuka kutoka eneo ambalo kituo cha polisi kiko mjini humo.
Jeshi la Nigeria halijatoa taarifa zozote kuhusiana na shambulio hiloambapo Awali wanawake wanne walipuaji wa kujitolea kufa walijilipua katika mji ulioko karibu wa Maiduguri, na kusababisha vifo vya watu wawili.
Jimbo la Borno, limekumbwa na maafa mabaya na uhasama kati ya majeshi ya serikali na Boko Haram kwa muda wa miaka minane sasa
Boko Haram ni kundi la Waislamu wenye itikadi kali kaskazini mwa Nigeria ambalo lina mwelekeo wa kijihadi na hutumia mbinu za kigaidi katika kuekeleza mashambulizi yake .
Boko Haram ilianzishwa na Yusuf Mohamed mwaka 2002 na inalenga kuanzisha dola la Kiislamu katika Nigeria ambako ni sheria ya pekee
0 comments:
Post a Comment