Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Quality Group Limited,
Bwana. Nicholas Ralph leo Machi 15.2017, amekutana na vyombo vya habari na kuelezea mipango mbalimbali ya
kampuni hiyo ikiwemo miradi yake inayoendeshwa karibu nchi nzima Tanzania Bara
na Visiwani.
Akizungumza na vyombo mbalimbali katika tukio lililofanyika majira ya Alasiri
ya leo Machi 15, Mkurugenzi huyo ameweza kuweka bayana miradi yao hiyo pamoja
na muelekeo wa kampuni katika kufikia malengo yake huku akibainisha kuwa, wataendelea kufanya
kwa kiwango cha hali ya juu ikiwemo kuwafikia wananchi kama sera ya makampuni
hayo na ile ya Taifa huku wakiungana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Dk. John Magufuli ya kupiga vita rushwa
na kuifanya Tanzania ya Viwanda.
Akielezea muelekeo wa kampuni hiyo amebainisha kuwa
watanzania wanaimani nao hivyo wataendelea kujikita zaidi kwenye miradi na
kuwafikia watanzania sehemu mbalimbali kama dira yao ya kuiletea Tanzania
maendeleo yaani 2016/2021 na ile ya mpaka 2025
“Quality Group imeweza na inaendelea kushirikiana na
makampuni yenye majina makubwa Duniani kwa kufanya nao kazi pamoja na uwakala
kwa hapa Tanzania ikiwemo kampuni za GM, Hoda,Isuzu, Bridgestone pamoja na Chevrolet
huku yakizalisha faida maradufu hii ni pamoja na kutoa ajira kwa
watanzania” amesema Mkurugenzi huyo.
Aidha, akitaja baadhi ya miradi ambayo inasimamiwa na
kampuni hiyo hapa nchini ni pamoja na mradi wa shamba la mpunga lililopo Mkoani
Morogoro ambalo litakuwa likipanda mazao hayo sambamba na kununua kwa wakulima
wadogowadogo ili kupata mchele.
Quality Group pia inasimamia miradi Visiwani Zanzibar
ikiwemo ule wa Stone Town Village huku pia mirad mingine ni ule wa Matrekta ambao ni wa Sonalika.
Kampuni hiyo kwa hapa nchini ni ya miaka mingi zaidi ya
miaka 30 huku ikiwa imeweza kuajili wafanyakazi zaidi ya 667,300 huku
ikitengeneza zaidi ya faida Bilioni 348.6 huku wa miongoni mwa makampuni
bora na yenye majina makubwa kwa kujijengea heshima ndani na nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment