Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Jaji (R ) Mbarouk Salum Mbarouk
Mkurugenzi
wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia
Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R ) Mbarouk Salum Mbarouk (wa
pili kushoto) akiwa na Wajumbe wa Tume Jaji (Mst.) Mary Longway na Mhe. Asina
Omari (kulia) wakiwa an Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia (kushoto)
wakifuatilia mada.
Na
Wandishi wa NEC, Dodoma
Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mbarouk Salum Mbarouk
amewataka wasimamizi wa uchaguzi na
wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria
zinazosimamia uchaguzi nchini katika kusimamia uchaguzi mdogo wa udiwani katika
kata 32 unaotarajiwa kufanyika Juni 15 mwaka huu.
Jaji
Mbarouk ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi kwa
wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka kata 32 na
halmashauri 20 za Tanzania Bara zinazotarajia kushiriki katika uchaguzi huo,
yanayofanyika jijini Dodoma.
Alisema
pamoja na baadhi ya wasimamizi kuwa na uzoefu katika kusimamia chaguzi
mbalimbali, aliwasisitiza kuzingatia maelekezo watakayopewa na Tume katika
kusimamia uchaguzi huo badala ya kusimamia kwa mazoea kwani NEC imewaamini kuwa
wanaweza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria.
“Ndugu
washiriki mnatakiwa kutambua kuwa mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu mnao uwezo
wa kufanya kazi hii jambo la muhimu ni kujiamini na kujitambua na kwamba
mtapaswa kuzingatia sheria, miongozo, kanuni na maelekezo yanayotolewa na Tume
kwa ajili ya kuendesha na kusimamia chaguzi” alisema Jaji Mbarouk.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt. Athumani Kihamia aliwataka
wasimamizi hao wa uchaguzi kuwepo muda wote wakati wa kutekeleza majukumu ya
uchaguzi na hata pale inapotokea dharura wahakikishe anakuwepo msimamizi
atakayetekeza majukumu yao.
“Ni
vyema mkafahamu kwamba kipindi hiki ambacho mmeshateuliwa na kuapa kuwa wasimamizi
wa uchaguzi, wewe unakuwa mtumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa muda
huo.Kwa hiyo ni vyema ukawa ofisini muda wote ukiondoa dharura” alisema Dkt.
Kihamia.
Alifafanua
kuwa suala hilo limetolewa muongozo katika Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015
sehemu ya 4 (1), watendaji wote wa uchaguzi katika kipindi cha uteuzi wa
wagombea, katika kipindi cha upigaji kura na katika hatua yoyote ya mchakato wa
uchaguzi.
Katika
mafunzo hayo, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi
walikula kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa mbele ya Hakimu Arnold
Kirekiano ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kuhusu hatua mbalimbali za
mchakato wa uchaguzi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment