METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 22, 2017

KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI MANISPAA YA UBUNGO YATEMBELEA MRADI WA UWEKEZAJI WA UGANDA AVENUE

Mwenyekiti wakamati ya fedha na uongozi Manispaa ya Ubungo ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akimsikiliza kwa makini Katibu wa kamati hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa mchanganuo wa namna ya mgawanyo wa fedha unavyokuwa kwa Manispaa yaKinondoni na Ubungo
 Msimamizi wa Mradi huo akimsikiliza kwa makini Meya wa Manispaa ya Ubungo alipokuwa akiuliza maswali kutaka kujua changamoto za uendeshaji wa mradi huo
 Wajumbe wa Kamati ya fedha na uongozi Manispaa ya Ubungo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo mara baada ya kukagua mradi wa uwekezaji wa Uganda Avenue

Kamati ya Fedha na Uongozi ya Manispaa ya Ubungo Leo Machi 21, 2017 imefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea Mradi wa Uwekezaji Plot No 188 Uganda Avenue Msasani Jijini Dar es salaam.

Ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob sambamba na Katibu wake ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo imezuru katika mradi huo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali za uwekezaji zinavyofanyika sambamba na kubaini hali ya ukusanyaji mapato na matumizi yake.

Katika mradi huo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina gawio la asilimia 40% ambapo Manispaa ya Kinondoni yenye inachukua asilimia 60%.

Katika mradi huo Mwekezaji baada ya kutoa pesa zake za gharama ya uendeshaji pesa inayobaki ambayo ni faida anaigawa kwa Manispaa ya Kinondoni na Ubungo ambayo ni asilimia 25% huku asilimia (75% anachukua yeye.

Asilimia hizo 25% zinazotolewa kwa ajili ya Manispaa hizo mbili ambapo zinaungwanishwa na kuwa asilimia 100%, zinagawanywa tena ambapo asilimia 60% inachukuliwa na Manispaa ya Kinondoni na asilimia 40% inachukuliwa na Manispaa ya Ubungo.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com