Wakati serikali kupitia jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wakijitahidi kutoa elimu ya usalama na matumizi sahihi ya barabara bado kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali za barabarani ambapo leo basi lenye namba za usajiri T636AWC mali ya kampuni ya RUKSA CLASSIC likitoka jijini
Mwanza kwenda Mkoani Kigoma limegongana uso kwa uso na gari dogo lenye
namba za usajiri T 210 DJJ katika kijiji cha Nhelegani mkabala na chuo
cha Ushirika Moshi kambi ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.
Ajali giyo imetokea majira ya nne asubuhi huku chanzo chake kikielezwa kuwa
ni uzembe wa dereva wa gari ndogo ambaye hakuwa na utulivu barabarani
na kujikuta yupo upande usio sahihi na kusababisha ajali.
Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa dereva wa gari dogo na
abiria wake mmoja, wameumia na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa mkoa
wa Shinyanga.
MASHUHUDA WAKIANGALIA AJALI HIYO
HAPA GARI ILIYOSABABISHA AJALI IKIWA KATIKA HALI MBAYA
0 comments:
Post a Comment